Wednesday , 17 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Profesa Assad aeleza siri ya jina lake
Habari Mchanganyiko

Profesa Assad aeleza siri ya jina lake

Aliyekuwa kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali ya Tanzania (CAG), Profesa Mussa Assad
Spread the love

 

ALIYEWAHI kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali ya Tanzania (CAG), Profesa Mussa Assad amesema, amekuwa anatumia jina la Mussa ambalo si la kwake kwa kipindi kirefu. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Leo Jumatano, tarehe 6 Oktoba 2021 jijini Dodoma, akizungumza katika mdahalo wa kuchambua Kitabu cha Rai ya Jenerali Ulimwengu na masuala ya Katiba, alianza kwa kusema “leo nitazungumza kitu ambacho sijawahi kukusema popote.”

Katika mdahalo huo ulioandaliwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Profesa Assad baada ya kukaribishwa kusema machache, alianza kwa kushukuru kwa fursa hiyo ya kualikwa kuwa mmoja wa wazungumzaji.

Profesa Assad amesema, ningependa niseme jambo ambalo sijawahi kulisema popote, “Mussa si jina langu mimi, jina alilonipa baba yangu ni Jaffar.”

“Wakati nasoma, kipindi kile kulitokea matatizo fulani fulani, ikabidi nitoke sehemu moja kwenda nyingine ili kumaliza masomo na hili jina la Mussa nikalipata huko ila watu wanaonifahamu wananijua kama Jaffar.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Sekta binafsi yasifu utekelezaji wa Mkumbi

Spread the loveSERIKAL imepongezwa kwa utekelezaji wa mapendekezo ya sekta binafsi kupitia...

Habari Mchanganyiko

Kamati ya bunge yapigia chapuo kilimo ikolojia

Spread the loveSERIKALI kupitia Wizara ya Kilimo imeshauriwa kushirikiana na wadau wa...

Habari Mchanganyiko

Serikali yapata hasara 113 milioni hospitali kuwapa misamaha wagonjwa wasiostahili

Spread the loveSERIKALI imepata hasara ya kiasi cha Sh. 111.76 milioni, baada...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC, Yanga wazindua kadi  za kimataifa za uanachama

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kushirikiana na Klabu...

error: Content is protected !!