Tuesday , 5 December 2023
Home Kitengo Maisha Elimu Prof. Ndalichako anusa harufu ya ufisadi Kagarwe
Elimu

Prof. Ndalichako anusa harufu ya ufisadi Kagarwe

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako akikagua chuo cha Ufundi Karagwe

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako, amemwagiza Mwenyekiti wa Bodi ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Peter Maduki kuunda tume ya kuhakiki matumizi ya Sh.4.65 bilioni katika ukarabati na ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi Karagwe Mkoa wa Kagera. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kagera … (endelea).

Profesa Ndalichako ametoa maagizo hayo hivi karibuni baada ya kukagua ukarabati na ujenzi  unaoendelea  wa chuo hicho ambao umepangwa kutumia kiasi hicho cha fedha mpaka utakapokamilika.

Chuo hicho kimekabidhiwa kwa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe ili iweze kukisimamia na kukiendesha.

Ametaka uhakiki huo ufanyike ndani ya kipindi cha wiki mbili (siku 14) ili kuokoa fedha hizo ambapo mpaka sasa Mkandarasi ambaye ni Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), ameshalipwa Sh.2.228 bilioni sawa na asilimia 48 ya gharama ya mradi huku mshauri elekezi EZM Architects and Associates akiwa amelipwa Sh.130.89 milioni.

Profesa Ndalichako amesema, baada ya kutembelea majengo haya na kuangalia gharama “sijaridhishwa kabisa, nikiangalia majengo haya, sijaridhika kabisa. Hatujawatendea haki watu wa Karagwe. Ikizingatia majengo yamejengwa kwa tofali za kuchoma ambalo moja ni Sh.80, kweli Sh.4 bilioni hapa, tumwogope Mungu.”

“Hapa sioni thamani ya fedha zilizokuja na majengo, ninakuagiza mwenyekiti na bahati nzuri fedha nyingi haijalipwa, fanya uhakiki ndani ya wiki mbili na bahati nzuri anayejenga ni TBA ambaye ni serikali. Ukaguzi ufanyike,” amesema Profesa Kabudi.

Waziri huyo amesema, Serikali imejenga na kukamilisha jumla ya Vyuo vya Mafunzo ya Ufundi Stadi 41 huku vingine 29 vikiendelea kujengwa nchini, lengo ni kufanikisha mkakati wa kujenga uchumi wa viwanda na kufikia Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2025.

Amewataka wananchi kutambua umuhimu wa mafunzo ya ufundi stadi na kuwahamasisha vijana kujiunga na mafunzo hayo ili waweze kujipatia ajira kwa urahisi na kujikwamua kiuchumi lakini pia kuchangia juhudi za serikali kwa kuchangia pato la Taifa  kwa kulipa kodi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari Mchanganyiko

CEO NMB awataka vijana kunoa ujuzi wao

Spread the loveAfisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna, amewashauri...

Elimu

150 wahitimu Shahada ya Udaktari HKMU

Spread the loveCHUO Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki (HKMU), kimeiomba serikali...

Elimu

Aliyehitimu udaktari HKMU na miaka 21 atoa siri

Spread the love MHITIMU wa fani ya udaktari ambaye ni mdogo kuwahi...

Elimu

Janeth Mbene apongeza HKMU, ataka wahitimu wajiajiri

Spread the loveWAHITIMU wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki (HKMU), ...

error: Content is protected !!