December 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Prof. Ndalichako aanika matumizi mabilioni ya fedha za UVIKO-19, aonya wafujaji

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia nchini Tanzania, Profesa Joyce Ndalichako

Spread the love

 

WIZARA ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, imepanga kutumia mabilioni ya fedha zilizotokana na Mpango wa Serikali wa Kuinua Uchumi na Kukabiliana na Ugonjwa wa Korona (UVIKO-19), kuimarisha maeneo matatu ya sekta hiyo. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Hayo yamesemwa hayo leo Jumamosi, tarehe 23 Oktoba 2021 na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako, akitoa mchanganuo wa matumizi ya fedha hizo, baada ya mpango huo unaogharimu Sh. 1.3 trilioni, kuzinduliwa na Rais Samia Suluhu Hassan, tarehe 10 Oktoba mwaka huu.

Prof. Ndalichako ametaja maeneo hayo ambayo wizara yake itashirikiana na Wizara ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI, la kwanza ni uimarishaji ujifunzaji na ufindishaji wanafunzi wenye mahitaji maalum, ambalo litagharimu Sh. 1.4 bilioni.

Katika eneo hilo, Waziri huyo wa elimu amesema, Sh. 707 milioni zitatumika kuchapa vitabu kwa ajili ya wanafunzi wenye uoni hafifu, Sh. 770 milioni, zitatumika kununua vifaa saidizi, ikiwemo bajaji, vishikwambi na kompyuta mpakato, kwa ajili ya wanafunzi 400 wenye mahitaji maalum waliko kwenye vyuo vikuu 11.

Prof. Ndalichako ametaja eneo la pili, kuwa ni uimarishaji mafunzo ya ufundi stadi na kwamba Serikali imetenga Sh. 57.9 bilioni, ambapo Sh. 28.7 bilioni zitatumika kununua vifaa vya kufundishia na kukamilisha ujenzi wa vyuo vya ufundi stadi 25 vya wilaya.

“Serikali imepanga kukamilisha ujenzi na kuweka samani, katika vyuo vinne vya ufundi stadi ngazi ya mikoa na mikoa itakayonufaika ni Njombe, Rukwa, Simiyu na Geita. Ambapo Sh. 18.7 bilioni kitatumika kwa ajili ya shughuli hiyo. Kukamilika kwa veta hizo kutaongeza nafasi za wanafunzi 5600,” amesema Prof. Ndalichako.

Eneo la tatu lililotajwa na Prof. Ndalichako, ni uimarishwaji mzingira ya utoaji elimu ya ualimu ambapo zimetengwa Sh. 5.4 bilioni.

Prof. Ndalichako amesema, Serikali imepnga kutumia Sh. 1.4 bilioni kujenga mabweni katika Chuo cha Ualimu wa Ufundi Morogoro. Wakati Sh. 6.8 bilioni zikipangwa kuimarisha vyuo vya maendeleo ya wananchi 34, kwa kununua vifaa vya kujifunzia na kufundishia.

Huku Sh. 266 bilioni zikitengwa kwa ajili ya kukiimatisha Chuo cha Ufundi Arusha, kwa kujenga jengo la taaluma litakalokuwa na kumbi za mihadhara, vyumba vya madarsa saba, ofisi 26, ambalo luitahudumia wanafunzi 911 na walimu 81 kwa wakati mmoja.

“Katika kuimarisha mazingira ya uandaaji walimu na kuongeza fursa ya upatikanaji elimu ya ualimu, katika mpango huu Serikali imepanga kujenga vyumba vya madarasa kwa jaili ya vyuo vya elimu, madarasa 41, kumbi tatu za hadhara na mabweni 15 na kuweka samani katika majengo hayo, utagharimu Sh. 5.4 bilioni,” amesema Prof. Ndalichako.

Waziri huyo wa elimu, ameagiza watumishi wa wizara hiyo kukamilisha mpango wa matumizi ya fedha hizo yakamilike ifikapo tarehe 30 Oktoba 2021, na kwamba hadi tarehe 30 Mei 2022 miradi hiyo iwe imeshakamilika.

“Miradi hii ikamilike kabla au ifikapo tarehe 30 Mei 2022, nataka kuona miradi yote itakayotekelezwa chini ya mpango huu iwe imaekamilika kabla Mei 2022, nataka kuona matokeo ya utekelezaji miradi hii inaendana na thamani ya fedha zilizotengwa,” amesema Prof. Ndalichako.

Wakati huo huo, Prof. Ndalichako amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Dk. Leonard Akwilapo, kuandaa mfumo wa uratibu, usimamizi na ufuatiliaji wa miradi hiyo ili kubaini changamoto zitakazojitokeza na kuchukua hartua stahiki kwa wakati.

Prof. Ndalichako amewaagiza watumishi watakaosimamia utekelezwa miradi hiyo kutoa taarifa kwa njia ya maandishi kila mwezi.

Waziri huyo wa elimu ameonya kuwachukulia hatua ikiwemo kuwafukuza kazi, watumishi watakaobainika kufuja fedha za miradi hiyo.

“Napenda kukumbushia fedha za mpango huu hazihusishi kulipana posho. Vitu viende na bei ya soko ukiniletea mpango wako wa maandalizi ukiwa na bei za ajabu ajabu, mpango wa maandalizi utakuondoa kwenye ofisi,” amesema Prof. Ndalichako na kuongeza:

“ Naomba tuelewane vizuri, usitujaribu. Mkuu wa idara lazima ujiridhishe bei tunazoletewa zinaendana na bei ya soko, hatutaki ujanjanja wa manunuzi.”

error: Content is protected !!