July 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Prof. Muhongo: Tutawanyang’anya

Spread the love

 

KAMPUNI na watu walio na maeneo ya uchimbaji madini ambao wameshindwa kuyafanyia kazi, watanyang’anywa na serikali, anaandika Regina Mkonde.

 Baada ya kunyang’anywa maeneo hayo ya uchimbaji, watakabidhiwa wachimbaji watakaokuwa tayari kuyatumia ndani ya wakati husika.

Kauli hiyo imetolewa leo na jijini Dar es Salaam na Profesa Sospeter Muhongo, Waziri wa Nishati na Madini katika mkutano wa kutathimini hali ya uchimbaji na mahitaji ya madini ya makaa ya mawe na jasi (Gypsum) nchini.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya wachimbaji wadogo kulalamika kuwa, baadhi ya kampuni na viwanda kuagiza madini hayo kutoka nje ya nchi kwa kigezo kuwa yanayozalishwa nchini hayana viwango, ubora na hayatoshelezi kulingana na mahitaji yao.

“Wachimbaji wazawa wasioyafanyia kazi maeneo yao kwa muda mrefu, tutawanyang’anya kwa mujibu wa sheria, ikifika siku ya Jumatatu kila kamishna katika eneo lake alete orodha ya wenye leseni za uchimbaji wa madini ya jasi na makaa ya mawe, zinafanyiwa kazi na zisizofanyiwa kazi,” amesema Muhongo.

Pia amewaagiza maofisa madini wa mikoa na wilaya ambayo madini hayo yanapatikana kujua ubora na kiasi cha madini kilichopo katika maeneo hayo.

“Ninawataka wawakilishi wa wachimbaji madini, wanunuzi pamoja na viongozi wa wizara kuitisha mkutano siku ya jumatano ijayo ili kujadili changamoto zinazowakabili kwa lengo la kufikia muafaka ili wachimbaji wapate hamasa ya kuchimba madini kwa wingi na yenye ubora,” amesema.

Benjamin Juampaka, Kamishna wa Madini Kanda ya Kusini ameeleza changamoto zinazosababisha wachimbaji wadogo kutochimba madini, ikiwemo ya uhaba wa mtaji, kutokuwepo kwa mikataba ya biashara ya muda mrefu na kucheleweshewa malipo yao.

“Baadhi ya viwanda huagiza madini nje ya nchi kitendo kinachokatisha tamaa wachimbaji wa wadogo, kama malipo na mikataba ingekuwa inatolewa kwa wakati unaofaa madini yangechimbwa kwa wingi,” amesema.

Fred Mahobe, Kamishna wa Madini Kanda ya Kusini Magharibi amesema, ukosefu wa taarifa za kutosha za kijiolojia unaosababishwa na wachimbaji wadogo kushindwa mudu gharama za tafiti.

“Changamoto nyingine ni tozo zinazokera ambazo zinatozwa na mamlaka za vijiji na wilaya, kitendo hiki hukwaza wachimbaji na ndiyo sababu ya baadhi yao kushindwa kuzifanyia kazi leseni zao kwa muda mrefu.

error: Content is protected !!