Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Prof. Muhongo ataka Tanzania iwe na satelaiti yake
Habari Mchanganyiko

Prof. Muhongo ataka Tanzania iwe na satelaiti yake

Spread the love

MBUNGE wa Musoma Vijijini, Profesa Sospeter (CCM) ameshauri Serikali kufikiria kuwa na satelaiti yake kwaajili ya tafiti zake za masuala mbalimbali ya maendeleo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Prof. Muhongo ametoa ushauri huo Bungeni leo Jumatatu tarehe 11 Aprili 2022 wakati akichangia hoja bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara zake.

Amebainisha maeneo matano yanayotakiwa kuwekewa mkazo kwenye masuala ya utafiti ikiwemo ya masuala ya sayansi na teknolojia ya anga.

“Tukitaka kilimo bora , uvuvi, utalii lazima twende kwenye space sayansi na teknolojia. Wengi wakisikia space wanadhani ni kitu kikubwa sana cha kutisha hapana.

“Na tunahitaji kuwa na satelaiti…Kenya wana satelaiti, Uganda watarusha moja mwaka huu, Zambia watarusha moja mwakani, Rwanda wanayo moja, Misri wanazo tisa, Nigeria wanazo saba,”

Ameshauri watafiti na vyuo vya Tanzania lazima waanzishe program za shahada zinazojielekeza katika tasnia hiyo.

“Satelaiti sio kitu cha ajabu, tunazihitaji kwenye mawasiliano na hata mambo yetu ya hali ya hewa na madhara mengine ambayo yanaweza yakatupata,” amesisitiza.

Amesema mwaka 2020 nchi ambayo ilitumia fedha nyingi kwenye utafiti ni Ubelgiji na Sweden ambazo zilitumia asiimia 3.5 ya GDP zao.

Amesema mwaka 2006 nchi za Kiafrika zilipitisha azimio kule Sudani la kutumia angalau asilimia 1 ya pato la Taifa kwenye mambo ya utafiti.

Nchi nyingi za Afrika hazijafika huko waliokaribia ni Afrika Kusini, Kenya na Senegali na wao wako asilimia 0.8, Tanzania tupo asilimia 0.5,” amesema Muhongo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!