MBUNGE wa Musoma Vijijini, Prof. Sospeter Muhongo, ameshauri masuala ya elimu kusimamiwa na wizara moja badala ya wizara mbili, akisema suala hilo linachangia maendeleo yake kudorora. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).
Prof. Muhongo ametoa ushauri huo Jana Alhamisi, bungeni jijini Dodoma, akichangia Bajeti pendekezwa ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa 2023/24.
Prof. Muhongo amesema masuala ya elimu ya msingi na sekondari inapaswa kusimamiwa na wizara moja, huku akishauri iundwe Wizara ya Elimu, Sayansi, Utafiti na Uvumbuzi.
Kwa sasa masuala ya elimu yanasimamiwa na Wizara ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI.
“Elimu yetu iko na hali mbaya na hakuna wa kumalumi, muda umefika na pendekezo langu ni kwamba elimu ya msingi na sekondari kuipeleka Wizara Ofisi ya Rais TAMISEMI matokeo yake siyo mazuri na tumerudi nyuma. Nashauri masuala ya elimu yarudishwe Wizara ya Elimu,” amesema Prof. Muhongo.
Pia, Mbunge huyo wa Musoma Vijijini, ameshauri miundombinu ya elimu hususan madarasa, maktaba na maabara viboreshwe ili wanafunzi wapate elimu bora.
Leave a comment