January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Prof. Muhongo aibua madudu Tanesco

Spread the love

WAZIRI wa Nishati na Madini, Professa Sospeter Muhongo, ameibua madudu makubwa katika Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Mkoa wa Mwanza baada ya kubaini kuwepo kwa mitambo mibovu mitatu yenye uwezo wa kuzalisha megawati 18. Anaandika Moses Mseti, Mwanza

… (endelea).

Prof. Mulongo alibaini hayo leo wakati wa ziara yake aliyoifanya katika kituo cha Nyakato, Wilaya ya Ilemela jijini Mwanza, kinachozalisha na kusambaza umeme kwenye mikoa ya Mwanza, Geita na Musoma.

Waziri huyo pia ametoa mwezi mmoja kwa Tanesco kuhakikisha wanatatua mvutano uliopo kati yao na mkandarasi aliyejenga mitambo hiyo katika kipindi hicho na kwamba kama hawatatekeleza agizo hilo hatua zitachukuliwa kwa watakaobainika wanahusika na tatizo hilo.

Prof. Mulongo amesema kuhalibika kwa mitambo hiyo inatokana na mainjinia wa Tanesco wabovu ambao hawakuweza kubaini tatizo mapema kabla ya kupokea mradi kutoka kwa mkandarasi aliyejenga mitambo hiyo Machi 2012.

Amesema kuwa mitambo hiyo 10 ilianza kujengwa Machi 2012 na kukamilika Novemba 2013 na kati ya hiyo mitatu imeharibika kwa kipindi cha miaka miwili tangu ianze kufanya kazi jambo ambalo linasababisha Watanzania kuendelea kubaki katika wimbi la mgao wa umeme.

Prof. Mulongo alidai kuwa mitambo yote 10 ilighalimu kiasi cha Sh. 129 billioni kujengwa, na pia mitambo hiyo ilitarajiwa kuzalisha megawati  60 lakini kwa sasa inazalisha megawati 42 pekee kutokana na hiyo mitatu kuhalibika.

Hata hivyo amesema kuwa kuendelea kuhalibika kwa mitambo hiyo kunasababisha kuongeza kwa deni la Tanesco ambalo kwa sasa linakalibia Dora kimarekani 400 milioni.

“Tulikuwa tunadaiwa Dora za kimarekani 300 milioni na tulikuwa tumelipa dora 200 milioni na sasa hivi tulikuwa tunaenda kuchukua dola 100 milioni kabla hata hatumaliza deni la zamani tunadaiwa nyingine tena 300 milioni.

“Hili tatizo sio la Nyakato pekee hata kule Kilwa Somanga Fungu huko nako hivyo hivyo, mitambo ambayo tumeijenga mwaka 2010 ndani ya mwaka mmoja inaharibika tatizo hili tunataka kulielewa.

“Tunataka kuwafahamu hawa mainjinia ambao walikuwepo hapa Nyakato na kule Somanga Fungu na nimemuagiza Mkurugenzi mkuu, Mramba awaulize tatizo hili limesababishwa na nini ndani mwaka mmoja tunakabiziwa mitambo inaharibika,” amesema Muhongo.

Aidha amesema kuwa uingiaji wa mikataba wa Tanesco na wakandarasi kuna udhaifu mkubwa kwani mitambo mitatu haiwezi kuhalibika ndani ya miaka miwili na kuitaka Tanesco kuwa makini katika uingiaji wa mikataba.

Meneja wa Tanesco Kanda ya Ziwa, Amos Maganga amesema kuwa mahitaji ya mikoa mitatu ya Mwanza inahitaji megawati 80 ambapo Mwanza ni 48, Mara 24 na Geita ni 8 lakini zinazozalishwa ni 42 kwa sasa.

Meneja wa  Kituo cha Nyakato, Ernest Nzemya, amesema kuwa kuhalibika kwa mitambo hiyo haitokani na uendeshaji wa Tanesco bali ni wakandarasi waliopewa dhumuni la kujenga chini ya kiwango hivyo ifikapo januari mwakani muafaka utakuwa umepatikani.

error: Content is protected !!