MBUNGE wa Musoma Vijijini, Prof. Sospeter Muhongo, ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Musoma, mkoani Mara, kutumia mapato yake ya ndani kukamilisha miradi ya maendeleo iliyokwama. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mara … (endelea).
Prof. Muhongo ametoa wito huo Leo tarehe 12 Mei 2023, mkoani Mara.
Miongoni mwa miradi iliyokwama ni pamoja na, ujenzi wa Hospitali ya Wilaya inayojengwa kwenye Kitongoji cha Kwikonero, makao makuu ya halmashauri, pamoja na kurekebisha vituo vya Afya vilivyojengwa chini ya viwango.
“Halmashauri itekeleze ipasavyo miradi ya maendeleo ya wanakijiji kwa kutumia mapato ya ndani. Halmashauri yetu itambue michango ya wadau wa maendeleo ikiwemo ya mbunge na ya wanavijiji kwenye miradi ya maendeleo inayotekelezwa Vijijini,” amesema Prof. Muhongo.
Katika hatua nyingine, Prof. Muhongo ameitaka halmashauri hiyo ijiepushe kupata hati chafu, huku akitaka itoe maelezo ya kina kuhusu hati chafu zilizopatikana.
“Ripoti za matumizi mabaya ya fedha za umma zitolewe haraka,” amesema Prof. Muhongo.
Leave a comment