Friday , 9 June 2023
Home Gazeti Tangulizi Prof. Muhongo agawa msaada kwa wananchi waliokumbwa na mafuriko
Tangulizi

Prof. Muhongo agawa msaada kwa wananchi waliokumbwa na mafuriko

Spread the love

 

MBUNGE wa Musoma Vijijini, Prof. Sospeter Muhongo, ametoa msaada wa dharura ikiwemo vyakula, kwa wananchi walioathirika na mafuriko ya mvua jimboni humo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mara … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mbunge Jimbo la Musoma Vijijini, Prof. Muhongo ametoa msaada huo katika Kijiji cha Kusenyi, Kata ya Suguti, jana tarehe 4 Aprili 2023.

“Mbunge ametembelea Kijiji cha Kusenyi kutoa pole kwa waathirika wa mafuriko ya juzi na jana. Kushuhudia uharibifu uliotokana na mafuriko hayo na kugawa chakula cha dharura. Ametoa gunia 25 ya mahindi na maharage kilo 100,” imesema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imetaja vitongoji vilivyoathirika ikiwemo Nyabweke ambapo kaya 26 zimekumbwa na maafa hayo na kitongoji cha Kwikutu ambacho kaya 24 zimeathirika.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, tathmini ya uharibifu wa mafuriko hayo inaendelea kufanywa, ambapo matokeo ya awali yanaonyesha baadhi ya nyumba zimebomoka, baadhi ya kaya chakula chao kilichohifadhiwa kimesombwa.

Tathmini ya awali inaonyesha kuwa, chanzo cha mafuriko hayo ni ujenzi wa barabara ya lami yenye urefu wa kilomita tano, kutozingatia uwekaji wa njia za kutosha za kupitisha maji, pamoja na wakulima wa mpunga kuweka miundombinu inayozuia maji kutiririka kwenye mikondo inayoelekea ziwani.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Prof. Muhongo ametoa wito kwa wananchi na wadau wa maendeleo kuendelea kuwasaidia wahanga wa mafuriko hayo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaTangulizi

Ngoma bado mbichi mkataba wa Bandari

Spread the love  SAKATA la mkataba wa uendeshaji, uendelezaji na uboreshaji wa...

BiasharaTangulizi

Mkurugenzi TPA: Mkataba unaweza kuvunjwa

Spread the loveMKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA),...

BiasharaTangulizi

Mkurugenzi TPA: Mikataba ya utekelezaji bado haijasainiwa

Spread the loveMKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA),...

Habari za SiasaTangulizi

Maulid Mtulia: Kutoka ubunge hadi U-DAS

Spread the love ALIYEKUWA mbunge wa Kinondoni, kupitia vyama vya The Civil...

error: Content is protected !!