Wednesday , 29 March 2023
Home Kitengo Maisha Elimu Prof. Mkenda aagiza uchunguzi wa kina shule zilizofanya udanganyifu
Elimu

Prof. Mkenda aagiza uchunguzi wa kina shule zilizofanya udanganyifu

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda
Spread the love

 

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda, amemuagiza Kamishna wa Elimu kufanya uchunguzi wa kina kwa shule nne zilizobainika kufanya udanganyifu mkubwa katika mtihani wa kidato cha nne mwaka 2022. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mwanza … (endelea).

Prof. Mkenda amesema hayo alipokutana na wazazi na walezi wa wanafunzi waliofutiwa matokeo ya mtihani wa kidato cha nne 2022 wa Shule ya Sekondari Thaqaafa ya Jijini Mwanza kwa ajili ya kuwasikiliza.

Amezitaja shule hizo kuwa ni Cornelius ya Kinondoni Dar es Salaam, Thaqaafa ya Mwanza, Mnemonic ya Zanzibar na Twibhoki iliyoko Mara na kumtaka Kamishna huyo kuchukua hatua kali kulingana na ripoti ya uchunguzi huo.

Mkenda amesisitiza wazazi kuwalea watoto katika maadili ili watambue kuwa udanganyifu si mzuri na una madhara makubwa katika upande wa haki, maadili na weledi.

“Tunapowapeleka watoto shule tunataka wajifunze waelewe ili baadae waje watumikie taifa. Sasa mtu anakuja kuwa daktari au mhandisi au rubani kwa kuiba mtihani, madhara yake ni makubwa sana,” ameongeza Mkenda.

Mkenda amewapa pole wazazi na kuwataarifu kuwa mitihani hiyo imefutwa na hivyo kilichopo ni kurudia mitihani.

“Kuhusu kurudia mtihani tumewasikiliza maombi yenu, ninashukuru kuwa hamna anayesema ameonewa sote tunakubaliana kuwa kulikuwa na udanganyifu na hivyo niseme matokeo yamefutwa na kikubwa ni maombi ya kurudia mtihani. Hili tunalichukua tutawasiliana nanyi baada ya kulifanyia kazi kwani ni suala la kibajeti pia,” amefafanua Mkenda.

Naye Adam Malima, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, akiwa katika kikao hicho amesema Serikali haitalea shule zinazofanya udanganyifu wa mitihani na kuongeza kuwa wanafunzi wanatakiwa wapimwe kwa uwezo na sio kwa kudanganya.

Katika maelezo yao yaliyotolewa kupitia Mwenyekiti wa wazazi hao, Patrick Msagati wameomba Serikali kuwahurumia na kuruhusu matokeo kuachiliwa au kuwapa nafasi ya kurudia mtihani.

“Tunaomba Serikali ichukue hatua kali kwa shule kama hizi kwani zimetusababishia madhara makubwa sisi kama wazazi na watoto pia. Ikiwezekana shule hizi zifungiwe,” amesema Michael Zayumba, mmoja wa wazazi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari

Serikali yataka vijana  wajiunge na program atamizi ya biashara CBE

Spread the love  SERIKALI imewahamasisha vijana kujiunga na program atamizi inayotolewa na...

Elimu

Mfuko wa Jimbo Musoma Vijijini wamwaga mamilioni ujenzi maabara za sekondari

Spread the love  MFUKO wa Jimbo la Musoma Vijijini, Mkoa wa Mara,...

ElimuHabari

CBE yaanzisha Shahada 10 za Uzamili, CBE yajivunia wahitimu wanaoajirika

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimewataka wenye  kampuni na...

Elimu

Harambee ujenzi sekondari za Musoma Vijijini yashika kasi

Spread the love  HARAMBEE ya ujenzi na ukarabati wa shule za sekondari...

error: Content is protected !!