January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Prof. Mbarawa amteua Lomayani Le-kujan TAMESA

Spread the love

PROFESA Makame Mbarawa, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano amemteua Mhandisi Manase Lomayani Le-kujan kuwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TAMESA) kuanzia tarehe 18 Februali mwaka huu, anaandika Happyness Lidwino.

Taarifa iliyotolewa leo na Joseph Nyamhanga, Katibu Mkuu Ujenzi imeeleza kuwa, uteuzi huo unatokana na utenguzi wa Mhandisi Benedict Magesa aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa TAMESA uliofanywa jana na Prof. Mbarawa.

Prof. Mbarawa alitengua uteuzi wa Magesa kwa kushindwa kusimamia matengenezo ya magari na mitambo ya serikali.

Taarifa zaidi zinaeleza kwamba, Magesa atapangiwa kazi nyingine wizarani. Kabla ya uteuzi wake, Manase alikua Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Ufundi na Ushauri katika Wakala wa Ufundi na Umeme (TAMESA).

error: Content is protected !!