March 6, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Prof. Lipumba: Nipo tayari kung’oka CUF

Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahm Lipumba akizungumzia barua kutoka Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora

Spread the love

PROFESA Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), amefungua milango kwa mwanachama mwenye uwezo kujitokeza na kugombea nafasi aliyonayo sasa. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Kiongozi huyo ameeleza leo tarehe 25 Septemba 2018 mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaama na kwamba, wakati wa kutafuta viongozi wapya unajongea hivyo wanaotaka kuwania nafasi mbalimbali ikiwa ni pamoja na uenyekiti wanapaswa kujiandaa.

Prof. Lipumba amesema kuwa, hang’ang’anii madaraka na kwamba, atakayejitokeza kuwania nafasi hiyo lazima awe na uwezo na akubalike kwa wanachama.

“Sing’ang’anii madaraka, nitaondoka lakini anayetaka nafasi hii lazima awe na uwezo pia akubalike kwa wanachama,” amesema Prof. Lipumba na kuongeza;

“CUF ni chama kinachofuata demokrasia kwa uwazi wake. Mpaka sasa hakuna mtu aliyejitokeza kutaka nafasi ya uenyekiti ambaye atapitishwa na kugombea urais kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.”

Hata hivyo, amegusia taarifa za Katibu Mkuu wa chama hicho Maalim Seif Shariff Hamada kutaka kuhamia Chadema ambapo amesema, hata akihama, hatodhoofisha CUF Zanzibar kwa kuwa ndio ilipo mizizi ya chama hicho.

error: Content is protected !!