Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Prof. Lipumba- Mwaka 2001 Tulijitenga na Mkapa
Habari za Siasa

Prof. Lipumba- Mwaka 2001 Tulijitenga na Mkapa

Prof. Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa CUF akimzungumzia anavyomfahamu Marehemu Benjamin Mkapa
Spread the love

PROFESA Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), amesema baada ya mauaji ya Zanzibar mwaka 2001, walijitenga na Rais mstaafu Benjamin William Mkapa. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumzia uhusiano wa kiasia kati ya chama chake na Mkapa enzi za utawala wake kuanzia mwaka 1995-2005 amesema, uchaguzi mkuu wa mwaka 2000, uliacha majeraha ya uhusiano hasa visiwani Zanzibar.

Mwenyekiti huyo wa CUF, amesema hayo leo Jumamosi tarehe 25 Julai 2020 nyumbani kwa Mpaka, Masaki jijini Dar es Salaam ambapo watu mbalimbali wanafika kutoa mkono wa pole kwa Anna, Mjane wa Mkaa, ndugu, jamaa na marafiuki.

“Matatizo ya Zanzibar mwaka 2001 yalituweka mbali na Mkapa, lakini baadaye mahusiano yalirejea baada ya muafaka. Alianza kutukaribisha kwenye shughuli mbalimbali za kiserikali na sisi tulihudhuria,” amesema Prof. Lipumba.

Mwanasiasa huyo anasema, Mzee Mkapa alionyesha kujutia mauaji hayo yaliyotkea akiwa madarakani na kwamba, alijitahidi kutafuta muafaka jambo ambalo lilileta faraja.

Mauaji hayo ya Januari 26 na 27, 2001 yalitokana na maandamano yaliyofanywa na wafuasi wa CUF, wakipinga matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC).

 

https://www.youtube.com/watch?v=hvtYcG40Xds

Prof. Lipumba anasema, Mzee Mkapa anastahili kupongezwa kwa kuwa, mara baada ya mauaji hayo, alihakikisha suluhu inapatina jambo ambalo alilisimamia mwenyewe mpaka wakati wa kutiliana saini.

Prof. Lipumba anasema, Mzee Mkapa wakati anaingia mdarakani mwkaa 1995, nchi haikuwa vizuri katika upande wa uchumi na kwamba, kulikuwa na mfumuko wa bei, rushwa na ufisadi.

“Wakati anaingia madarakani, kiuchumi kulikua na tatizo likiwemo mfumuko wa bei, ufisadi na rushwa. Hata hivyo, alifikia makubaliano ya utaratibu wa namna ya kuimarisha,” amesema.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online, MwanaHALISI TV na mitandao yetu ya kijamii ya Twitter, Facebook na Instagram kwa habari mbalimbali

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!