October 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Prof. Lipumba kugombea urais Tanzania

Prof. Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa CUF

Spread the love

MKUTANO Mkuu Maalum wa Chama cha Wananchi (CUF), leo Jumatatu tarehe 27 Julai 2020, umempitisha Prof. Ibrahim Lipumba, mwenyekiti wa chama hicho kuwani urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa tarehe 28 Oktoba 2020. Anaripoti Yusuph Katimba, Dar es Salaam…(endelea).

Prof. Lipumba amepigiwa kura ya ndio 756 sawa na asilimia 96 ambapo wajumbe waliopiga kura ni 789 na kura 21 zimeharibika, kura ziizosema hapana 12 .

Matokeo hauo yametangazwa na, Wakili Mashaka Ngole, msimamizi wa uchaguzi huo.

Awali, Haroub Mohamed Shamis, Katibu Mkuu wa chama hicho alisema, kulikuwa na wanachama watatu waliochukua fomu ya urais, lakini wawili walijitoa kwenye kinyang’anyiro hicho na kumuacha Prof. Lipumba peke yake.

“Ni wanachama watatu ndio waliochukua fomu ya kuomba kugombea urais, lakini wawili kati yao walijitoa. Mimi sijui kwanini walijitoa. Kwa hiyo tuna mgombea mmoja,” amesema.

Wakati huo huo Wakili Ngole amemtangaza Musa Haji Kombo kuwa mshindi wakura 535 huku akifuatiwa na Mohammed Habib Mnyaa kwa kira 100 na wa mwisho ni Rajabu Mbarook Mohammed aliyepata kura 84.

Wakati kura zaote zilikuwa 734 ambapo kura halali zilikuwa 719 huku kura 15 zikiwa zimeharibika

error: Content is protected !!