Tuesday , 30 May 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Prof. Lipumba azidi kutokomezwa
Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba azidi kutokomezwa

Prof. Ibrahim Lipumba
Spread the love

HARAKATI za Prof. Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) kujiweka mbali na vyama shirika vya upinzani zinaelekea tamati. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Ni baada ya chama chake kuueleza umma kuwa, kinajiondoa rasmi kwenye Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA). Awali umoja huo ulikuwa ukiunda na vyama vine ambavyo ni CUF yenyewe, Chadema, NCCR-Mageuzi, NLD ambapo baadaye ACT-Wazalendo kilijumuishwa baada ya taratibu zao kukamilika.

Akizungumza na Kituo cha Televisheni cha EATV, Halifa Suleiman Halifa, Katibu Mkuu wa CUF amesema, chma chake kimekuwa ikitendwa hovyo na Chadema wakati kilipokuwa katikati ya mgogoro wa kiuongozi uliotikisa kwa miaka mine.

Amedai kuwa, baadhi ya wabunge wa Chadema walikuwa wanaingilia masuala ya ndani ya chama hicho jammbo lililochochea mgogoro.

Kiongozi huyo wa CUF amesema, haiwezi kushirikiana na Ukawa akidai kuwa, ushirikiano wa umoja huo ni wa kiadui na chuki, badala ya kuwa ushirikiano mzuri wa kisiasa.

“Walikuwa wazungumzaji wa wabunge wa CUF. Sisi wakati tuanenda mahakamani Chadema wanakuja kutufanyia fujo, ilkuwa inawahusu nini wakati yale yalikuwa matatizo ya ndani ya chama?” amehoji Halifa.

Hata hivyo, Halifa amesema umoja huo wa Ukawa upo hoi bin taaban na kwamba hadhani kama upo imara.

Kauli ya Halifa ilitanguliwa na ile ya Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema aliyoitoa tarehe 15 Machi 2019 kwamba, hawaitambui CUF Lipumba hivyo kuiweka pembeni kwenye umoja huo.

CUF imeendelea kutengwa wakati ambao wanachama wake wanakimbilia ACT-Wazalendo baada ya Maalim Seif kujiunga na chama hicho ambacho kwa sasa ni sehemu ya Ukawa.

Kuondoka kwa CUF Ukawa kunaendelea kumweka mbali Maalim Seif na Prof. Lipumba ambao wamekwaruzana kwa muda mrefu ndani ya CUF.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Uamuzi juu ya wakurugenzi kusimamia uchaguzi 13 Juni

Spread the love  MAHAKAMA ya Afrika ya Haki za Binadamu (ACHPR), imepanga...

Habari MchanganyikoTangulizi

Jeshi la Polisi kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika utafiti

Spread the love  JESHI la Polisi Nchini limesema kuwa katika kukabiliana na...

KimataifaTangulizi

Mtuhumiwa wa mauaji ya halaiki ya Rwanda akamatwa Afrika Kusini

Spread the love  MMOJA wa watuhumiwa wakuu wa mauaji ya Kimbari ya...

Habari za Siasa

Musoma Vijijini waomba ujenzi wa barabara uanze haraka

Spread the loveJIMBO la Musoma Vijijini, mkoani Mara, limeomba Serikali kuhakikisha ujenzi...

error: Content is protected !!