Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Prof. Lipumba awakumbuka waliouwawa kwenye maandamano
Habari za Siasa

Prof. Lipumba awakumbuka waliouwawa kwenye maandamano

Prof. Ibrahim Lipumba
Spread the love

IKIWA ni miaka 18 tangu kutokea kwa mauaji ya waandamanaji wa Chama cha Wananchi CUF visiwani Zanzibar, Profesa Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa chama hicho anayetambaliwa na msajili wa vyama vya siasa ameendaa maombi maalumu kwa ajili ya marehemu hao. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akizungumza na Waandishi leo Januari 26, 2019 kwenye Ofisi ya chama hicho Buguruni jijini Dar es Salaam ambapo ameeleza kuwa kesho tarehe 27 Januari 2019, kwenye viwanja cha Mnyamani kilichopo Buguruni wilani Ilala, chama hicho kitafanya maombi maalumu kwa ajili ya marehemu waliofariki kwenye maandamano hayo.

Prof. Lipumba amesema kuwa vurugu zilisababishwa na kuvurugika kwa uchaguzi wa mwaka 2000 ambao uliitia dosari Tanzania kwenye anga za kimataifa ambapo waangalizi wa uchaguzi wa nje na ndani na jumuiya ya nchi za Madola ilipendekeza kuundwa kwa tume huru visiwani humo na kurejewa kwa uchaguzi huo.

“Tume ya Uchaguzi Zanzibar iliamua kurejea chaguzi huo katika majimbo 16 ya Mjini Magharib pekee ili kuipa CCM ushindi kwenhe majimbi hayo,” amesema Prof. Lipumba na kuongeza.

“Baada ya kitendo hicho aliyekuwa Rais wakati ule awamu ya Tatu, Benjamini Mkapa alipiga marufuku mikutano ya hadhara na maandamano ya vyama vya siasa kwa madai kuwa Serikali ya CCM iwepe ya kutekeleza sera zake.”

Amesema kuwa agizo hilo la Rais Mkapa lilisimamiwa kidete na viongizi wote wa Serikali pamoja na kuungwa mkono Makamo wa Rais wa kipindi kile, Dk. Omari Ali Juma na Waziri Mkuu Fredrick Sumaye.

Prof. Lipumba amesema kuwa kufuatia hatua hiyo CUF kilitangaza maandamano ya amani nchi mzima kwa lengo la kudai Katiba mpya yenye misingi ya Demokrasia, Tume huru ya Uchaguzi, kurejewa kwa uchaguzi na kuwepo kwa utawala bora utakao heshimu Haki za Binaadamu.

Ameeleza kuwa kabla CUF haijapeleka barua ya taarifa ya maandamano hayo kwa Jeshi la Polisi Mkuu wa Mkoa wa wakati huo Yusuf Makamba, Waziri Mkuu Sumaye na Makamo wa Rais Dk Omary Ali Juma walipiga marufuku maandamano hayo.

Prof. Lipumba ameeleza kuwa baada ya kauli za viongozi wa serikali ilimlazimu siku ya tarehe 25 Januari, 2001 aende idara ya habari ya Maelezo kwa ajili ya kusisitiza kuwa maandamano ya CUF.

Amesema vuguvugu lilianza baada yeye kwenda kumuunga mkono mbunge wake aliyekuwa ameitisha mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Mbagara Zakhem ambapo Jeshi la Polisi lilivunja mkutano ule halali kwa nguvu na kuwapiga viongozi wa chama hicho na kuwatia mbaroni pamoja na yeye mwenyewe.

Prof. Lipumba amesema kuwa tukio la kwanza la mauji yaliyotelezwa na Jeshi la Polisi Visiwani Zanzibar la Tarehe 26 Januari, 2001 ambapo aliuawa kwa risasi Imami wa Msikiti wa Mwembe Tanga wilaya ya Mjini.

Amesema siku iliyofuata ya tarehe 27 Januari, 2001 ambayo haitasahaulika kwa wanachama wa CUF waliondamana kwa amani Visiwani Zanzibar Dar es Salaam na Uingereza waliojitokeza kwa wingi kuandamana.

Amesema wafuasi hao walioandama kwa amani walijikuta wakiangukia kwenye mikono ya Jeshi la Polisi waliokuwa wakitumia Risasi ambapo walipelekea mauaji ya watu 70 Unguja na Pemba pamoja na Dar es Salaam.

Pref. Lipumba ameeleza kuwa vurugu hizo zilisababisha kupoteza maisha kwa wananchi wengi kwa wakati mmoha tangu histori ya nchi huru kuanza na kwa mara ya kwanza nchi kuzalisha wakimbizi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Chadema yamtaka Rais Samia aunde tume kuchunguza mauaji mgodi wa Barick

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameombwa aunde tume huru kwa...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

error: Content is protected !!