November 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Prof. Lipumba awaangukia Wazanzibar

Prof. Ibrahim Lipumba

Spread the love

MWENYEKITI wa CUF Taifa, Profesa Ibrahim Lipumba amewaangukia wanachama wa chama hicho visiwani Zanzibar kumuunga mkono. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Prof. Lipumba ametoa wito huo leo tarehe 19 Machi 2019 wakati akizungumza na wanahabari  jijini Dar es Salaam.

Amewataka wanachama hao kutokuwa na jazba kufuatia hatua ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif harrif Hamad na baadhi ya wafuasi wake kuhamia chama cha ACT-Wazalendo

“Wito kwa wananchi, wanachama na hususan wa CUF Zanzibar, kwamba hiki ni chama kimoja, tuna chama kimoja waendelea kuunga mkono chama cha CUF tumetoka mbali kwenye kudai haki katika nchi yetu, sisi tuikuwa kipaumbele kudai haki ya kupata katiba mpya, tume huru ya uchaguzi, utawala bora,” amesema na kuongeza Prof. Lipumba

“Hakuna mtu aliyetetea haki za Wazanzibari kama Prof. Lipumba. Historia inaonyesha hakuna kama Profesa Lipumba, seif shariff asitufarakanishe, ubinafsi wa maalim seif ni hatari leo hii anahama anasema anakwenda act anawaambia wabunge nao wamfuate wanaowakilisha bunge.”

Aidha, Prof. Lipumba amesema kwa sasa ana kazi ya kuponya majeraha yaliyotokana na mgogoro wa kiuongozi wa CUF.

“Wazanzibar wasiinge jazba kuchoma bendera zozote ni kosa la jinai kubadilisha ofisi ya chama, ofisi ya mtendeni ni ya chama,” amesema Prof. Lipumba.

error: Content is protected !!