December 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Prof. Lipumba atwaa uenyekiti CUF

Spread the love

PROFESA Ibrahim Lipumba ametwaa nafasi ya uenyekiti wa chama hicho kwa mara nyingine. Anaripoti Bupe Mwakiteleko … (endelea).

Miongoni mwa majukumu ya leo katika Mkutano Mkuu wa CUF ni pamoja na kupata viongozi mbalimbali wa chama hicho.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi huo uliofanyika leo tarehe 12 Machi 2019, Thenei Juna Ally amesema, Prof. Lipumba amepata jumla ya kura 516 ikiwa ni zaidi ya asilimia 88 ya kura zote.

Thenei amemtangaza pia Maftaha Nachuma kuwa ameshinda nafasi ya Makamu Mwenyekiti Bara kwa kupata kura 231 sawa na asilimia 40 huku Makamu Mwenyekiti Visiwani akitajwa kuwa Abas Juma Muhunzi ambaye alipata kura 349 sawa na asilimia 60.9.

Prof. Lipumba baada ya kutangazwa kushinda amesema, walioshinda katika nafasi nyingine ni vijana wake na kwmaba, atakwenda nao vizuri katika kuongoza chama hicho.

Mkutano Mkuu wa chama hicho ulianza jana na untarajiwa kumalizika kesho tarehe 14 Machi 2019.

error: Content is protected !!