Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Prof. Lipumba atoa masharti kuungana na Mbowe, Zitto 
Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba atoa masharti kuungana na Mbowe, Zitto 

Prof. Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa CUF
Spread the love

PROF. Ibrahim Haruna Lipumba, mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), ametoa masharti mazito ya “ushirikiano” kwa viongozi wenzake wa vyama vya ACT- Wazalendo na Chama cha Demokarsia (Chadema), kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari, leo Jumatatu, makao makuu ya chama chake, Buguruni, Prof. Lipumba amesema, ili CUF iungane na Chadema na ACT- Wazalendo, ni sharti vyama hivyo, “visipokee mabaki” kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM). 

Amesema, “nipo tayari kuungana na Mbowe na Zitto Kabwe, pamoja na vyama vingine vya upinzani, iwapo watakuwa tayari kutekeleza sharti hilo. Vinginevyo, sisi kama CUF tutakwenda kivyetu na wao kivyao.”

Kwa mujibu wa Prof. Lipumba, CUF haiko tayari kuungana na vyama vinavyosubiria wagombea walioenguliwa na kuonekana hawafai katika nafasi mbalimbali ndani ya CCM.

Kiongozi huyo wa CUF ametoa msimamo huo, kufuatia kauli ya Zitto, kwamba vyama vya upinzani havina budi kuungana katika uchaguzi huo, ili viking’oe chama tawala madarakani.

Kupitia mkutano huo, Prof. Lipumba amesema vyama vya upinzania mpaka sasa havijazungumza chochote kuhusu ushirikiano huo.

“Huwezi sema ushirikiano wakati hujaongea na vyama. Unatakiwa ushirikiano wa kuitoa CCM madarakani na sio ushirikiano wa kusubiri mabaki ya CCM.

“Sio utaratibu wa kufanya umoja wa kusubiri nani atakeyetemwa na CCM au kuenguliwa. Tutashirikiana na vyama vyenye nia ya dhati ya kusimamia mabadiliko ya kweli,” ameeleza Prof. Lipumba.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!