January 25, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Prof. Lipumba apelekwa mahakamani kinyemela, aachiwa kwa dhamana

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Prof. Ibrahim Lipumba akiwa chini ya ulinzi kwenye gari la polisi muda mcheche baada ya kukamatwa

Spread the love

SINEMA nyingine imeibuka. Ni ndani ya siku 10 tangu ikamilike sinema iliyohusu mgogoro wa uongozi wa serikali ya mtaa wa Migombani, segerea wilaya ya Ilala Dar es Salaam. Anaripoti Pendo Omary.

Sinema mpya inamhusu Mwenyekiti Wa taifa Wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba. Ambaye jana aliongoza maandamano ya amani ya chama hicho yaliyolenga kuadhimisha kumbukumbu ya mauaji ya kikatili ya wana-CUF ya 26-27 Januari Miaka 14 iliyopita.

Sinema ya Migombani ilimalizika Kwa serikali ya CCM kusalimu amri kwa kuheshimu maamuzi ya wanannchi waliomchagua Kwa kura nyingi Japhet Albert aliyegombea uenyekiti wa mtaa huo kwa CHADEMA.

Kembo aliapishwa na Mwanasheria wa serilali 17 Januari 2015, ikiwa no siku tatu tokea alipoapishwa kwa nguvu ya wananchi kupitia kwa wakili wa kujitegemea.

Prof. Lipumba leo mchana alisomewa shitaka moja la kudaiwa kuchochea watu kutenda makosa ya jinai na kesi yake, kuhairishwa baada ya yeye kupewa dhamana ya wadhamini wawili.

Wakili Peter Kibatala ambaye aliongoza jopo la mawakili sita, ameiambia MwanaHALISIonline leo jioni kwamba kesi hiyo itafikishwa mahakamani 26 Februari Kwa ajili ya kutajwa.

Hakika ni sinema mpya inayozidi kuonesha kuwa safari ya kujenga demokrasia ya vyama vingi nchini Tanzania ni ndefu, ngumu Na imejaa misukosuko ya kila aiana.

Uongozi wa CUF kupitia ofisi yake ya wilaya ya Temeke ilipeleka taarifa kwa mkuu Wa polisi wilaya, zaidi ya wiki moja iliyopita kujulisha ratiba ya maandamano ya amani kuanzia Temeke Mwisho na kuishia viwanja vya Mbagala Zakhem kwa mkutano wa hadhara.

Hakukuwa na taarifa yoyote ya msimamo wa Jeshi la Polisi. Kwa kawaida utaratibu ni kwamba maandalizi yaendelee kwa kuwa hakuna pingamizi lolote. Lakini Jumatatu usiku uongozi wa CUF ulipokea barua ya kupiga marufuku maandamano na mkutano.

Wakati huo matangazo ya ratiba hiyo yalishaenea Dar es Salaam nzima na mikoa ya jirani. CUF ambayo ilikuwa na ratiba kama hiyo ya maandamano ya amani na mkutano kisiwani Pemba ambako vyombo vya dola viliuwa zaidi ya waandamanaji 30 siku ya 27 Januari, 2001 hawakufuta ratiba yao.

Prof. Lipumba aliyevalia fulana nyekundu na kosia zenye nembo ya CUF na suruali nyeusi, alifika Temeke mwisho na wasaidizi wake kutoka makao makuu na wilaya ya Temeke mnamo saa nane mchana. Umma ulikwisha kusanyika yapata Mita 100 polisi wa kutuliza ghasia wakiwa kwenye magari matano ambao walivaa silaha nzito nzito walikuwa wamejiandaa kufanya walicho kipanga.

Mwenyekiti huyo Wa CUF alipanda juu ya gari la wazi akashika kipaza sauti na kutangazia umma kuwepo barua ya polisi kuzuia maandamano ya amani.

Akasema kwamba wakati wao wanayo taarifa hiyo wenzao waliokuwa tayari kwenye viwanja vya Mbagala Zakhem hawakiwa na taarifa hiyo. “Tunapaswa kuwafuata ili nao wapate taarifa hii mpya wasioitarajia,” alisema.

“Nakuombeni sana Kwa kuwa tumekusudia kuandamana kwa amani na serikali haitaki tawanyikeni kwa amani wakati Mimi na viongozi wenu wengine tukienda Mbagala kutoa taarifa hii kwa wenzenu,” Prof. Lipumba aliongeza.

Wakati msafara huo unaondoka Temeke Mwisho magari ya polisi aina ya Land Rover 110 na kuanza kufyatua mabomu ya machozi na risasi za mipira na kuzua tafrani kubwa katika eneo hilo linalojaa watu muda wote.

Polisi wa FFU wakaanza kuwakamata wafuasi wa CUF na hasa viongozi waliofuatana na Prof ambaye na mwenyewe alikunjwakunjwa na ‘mapolisi’ wa miraba minne. Zaidi ya viongozi 30 wakiwemo walinzi wa viongozi Wa CUF walikamatwa na wote kupelekwa lituo Kikuu cha kanda maalum ya polisi (Central).

Baada ya kuachiwa kwa dhamana ya maandishi jana usiku, Prof. Lipumba na viongozi wote wengine walitakiwa kuripoti saa nne asubuhi Leo.

Waliachiwa ili kurudi kesho kwa ajili ya kupelekwa mahakamani. Ghafla, na hasa baada ya wabunge wa UKAWA kuibana serikali kupitia bunge Iitoe kauli kuhusu ukandamizaji wa haki za wananchi kwa kuzingatia tukio hilo, Prof Lipumba alikamatwa tena na kurudishwa kituoni.

Hatimaye amepelekwa mahakamani leo saa tisa Alasiri kusomewa shitaka moja, hatua ambayo wachambuzi wa siasa za Tanzania wanaielezea kuwa ” ni njama ya serikali ya CCM kuzima joto la Kambi ya Upinzani bungeni iliyombana Spika Anna Makinda kusitisha shughuli za bunge ili kujadili ukandamizaji wa haki zawananchi jijini Dar es Salaam.”

Kutokana na mvutano ulioibuka bungeni, uliozaa mtafuruku Spika aliahilisha bunge ghafla kwa ahadi kwamba serikali itoe taarifa rasmi bungeni kesho.

error: Content is protected !!