Thursday , 2 February 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Prof. Lipumba apangua wakurugenzi CUF
Habari za Siasa

Prof. Lipumba apangua wakurugenzi CUF

Prof. Ibrahim Lipumba
Spread the love

 

MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba amefanya mabadiliko madogo ya wakurugenzi wa chama hicho. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Prof. Lipumba amefanya mabadiliko hayo leo Jumatatu, tarehe 23 Agosti 2021.

“Baada ya kushauriana na Makamu Mwenyekiti wa Tanzania Bara, Maftah Nachuma na Kaimu Makamu Mwenyekiti wa Zanzibar, Mussa Haji Kombo, nimefanya mabadiliko madogo ya wakurugenzi,” imesema taarifa ya Prof. Lipumba.

Katika mabadiliko hayo, Prof. Lipumba amemteua Khamis Mohamed Faki, kuwa4 Naibu Mkurugenzi wa Habari.

Taarifa ya uteuzi huo imesema, Faki anachukua nafasi ya Mbarouk Seif Salim ambaye ni Kaimu Naibu Katibu Mkuu.

Pia, Prof. Lipumba ameteua Rajab Mbarouk Mohamed, kuwa Mkurugenzi na Katibu wa Kamati ya Itifaki na Udhibiti, akichukua nafasi ya Thinney Juma Mohammed, ambaye anabaki na jukumu la kuwa mshauri wake maalum.

“Uteuzi huu utafikishwa kwenye kikao kijacho cha Baraza Kuu la Uongozi la Taifa kwa kuthibitishwa,” imesema taarifa ya Prof. Lipumba.

Taarifa ya Prof. Lipumba imesema, amefanya uteuzi huo kwa mujibu wa katiba ya CUF, toleo la 2014 Ibara ya 91 (1) (f), inayompa mamlaka ya kufanya hivyo kwa kushauriana na makamu mwenyekiti.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kamati ya Bunge yaitaka Serikali ichukue hatua kudhibiti mfumuko wa bei

Spread the love  SERIKALI ya Tanzania imetakiwa kufanya tathimini dhidi ya changamoto...

Habari za Siasa

Bunge lataja kinachokwamisha Mradi wa Mchuchuma na Liganga

Spread the love  MRADI wa uchimbaji chuma cha Liganga na Makaa ya...

Habari za Siasa

Chongolo aagiza watendaji wanaoonyesha mianya ya rushwa wakamatwe

Spread the love   KATIBU mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa...

Habari za Siasa

TRA iweke mfumo wa msamaha wa kodi kutekeleza miradi

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Taifa kimeitaka Mamlaka ya Mapato...

error: Content is protected !!