Monday , 22 April 2024
Home Gazeti Mpya Prof. Lipumba amtumia Lowassa kujiimarisha
MpyaSiasa

Prof. Lipumba amtumia Lowassa kujiimarisha

Spread the love

PROFESA Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, ameanza kumtumia Edward Lowassa aliyerejea CCM kujiimarisha kisiasa. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Kiongozi huyo aliye kwenye siasa za upinzani kwa zaidi ya miaka 20 ameanza kumwaga hadharani mazungumzo ya vikao vya ndani vilivyofanywa na viongozi wakuu wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kabla ya kuingia kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2015 huku akituhumu kuwa, viongozi wenzake walimpuuza.

Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 6 Machi 2019 katika ofisi kuu ya chama hicho iliyopo Buguruni jijini Dar es Salaam amesema kwamba, Lowassa hakujiunga Ukawa kupitia Chadema kutekeleza malengo ya umoja huo (Ukawa).

Prof. Lipumba amesema, “ni wazi Ndugu Lowassa aliingia Chadema baada ya kutemwa CCM apate fursa ya kugombea urais na sio kutekeleza lengo la Ukawa la kujenga taifa la wananchi walioelimika na kujitambua, kutokomeza umasikini.

“Pia kutumia rasilimali za maliasili kwa manufaa ya wananchi wote, kupambana na rushwa na ufusadi na kuwa taifa lenye utu, uzalendo, uadilifu, umoja, uwazi na uwajibikaji.”

Amedai kuwa, hata kama Lowassa angechaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri, angeshughulishwa ama kuwasikiliza zaidi rafisiki zake ndani ya CCM akiwataja Rostam Azizi, aliyewahi kuwa Mbunge wa Igunga; Naziri Karamagi, aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini na wengine kutoka katika chama hicho na kuwa, asingewasikiliza viongozi wa Ukawa.

Kwenye mkutano huo amesema, kurejea kwa Lowassa CCM kunaonesha wazi kwamba alikuwa sahihi kutokumuunga mkono katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2015.

Prof. Lipumba lijiuzulu uenyekiti wa CUF baada ya vyama vinavyounda UKAWA kumteua Lowassa kuwa mgombea wa Urais.

Prof. Lipumba alijiuzulu akidai kuwa  umoja huo ulishindwa kuongozwa na maadili kwa kumteua Lowassa ambaye alikuwa katika kundi lililokuwa linapinga Rasimu ya Katiba ya Wananchi.

Leo Prof. Lipumba ameeleza kuwa, Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad alimficha kuhusu kikao cha faragha alichoketi na Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe akimshawishi kumkaribisha Lowassa kwa kuwa chama chake hakina mgombea.

Ameeleza kuwa, baada ya kupinga kuteuliwa Lowassa kugombea urais kupitia UKAWA, alishauriana na wakurugenzi wa CUF na kutangaza nia ya kugombea urais  na kutaka kuungwa mkono na vyama vya UKAWA, na kwamba hatua hiyo haikuwafurahisha Chadema.

Amedai kuwa, Maalim Seif na Mbowe waliitisha kikao cha wenyeviti na makatibu wakuu wa UKAWA kwa lengo la kumsulubisha ili ajitoe katika kinyang’anyiro cha kugombea urais.

Prof. Lipumba amesema alikutana na watu walioteuliwa awali kugombea Urais  kwenye vyama vyao, akiwemo Dr. George Kahangwa aliyeteuliwa kuiwakilisha NCCR-Mageuzi na Dk. Wilbroad Slaa aliyetakiwa kugombea kupitia Chadema. Katika kikao hicho walimteua Dk. Slaa kuipeperusha bendera ya UKAWA kwenye uchaguzi wa Urais wa mwaka 2015.

“Hata hivyo, Chadema walimtosa Dk. Slaa na kumkaribisha Lowassa kuwa mgombea Urais. Nilikuwa na wakati mgumu sana wa kufanya maamuzi.

“Nilikubali kumuunga mkono Dk. Slaa kuwa mgombea wetu wa UKAWA, sikuweza kumpigia debe Lowassa kuwa ndiye kamanda wetu wa kupambana dhidi ya rushwa na ufisadi ikanibidi ning’atuke, nilishambuliwa sana lowassa kurudi CCM kunaonyesha wazi nilikuwa sahihi kutokuwa mpiga debe wa Lowassa,” amesema Prof. Lipumba.

Tazama video kamili hapo chini

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

HabariSiasa

Dk. Rose Rwakatare atoa kadi 500 kila Wilaya Morogoro

Spread the loveMWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk...

Habari MchanganyikoSiasa

Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) waapishwa rasmi  

Spread the loveWABUNGE wa Bunge la Tano la Jumuiya ya Afrika Mashariki...

HabariSiasa

Vigogo ACT mbaroni kwa uchochezi, kukashifu viongozi wa Serikali

Spread the loveJESHI la Polisi Mkoa wa Kusini limewakamata na kuwahoji watu...

HabariSiasa

Shaka CCM tusipoteze muda  wa malumbano

Spread the loveKATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Itikadi...

error: Content is protected !!