July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Prof. Lipumba ampa rai Rais Magufuli

Spread the love

ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba, amemtaka Rais John Magufuli kuishauri Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kutangaza matokeo ya uchaguzi wa Zanzibar kabla ya kuhutubia bunge, Anaandika Faki Sosi … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari leo Ofisi Kuu ya chama hicho Buguruni jijini Dar es Salaam Prof. Lipumba amesema, ZEC imebakiza kuhakiki majimbo 14 ambapo haitachukua saa tatu katika kupitia majimbo hayo, na kwamba mpaka kufika kesho ataweza kuapishwa rais huyo.

“Tume ilihakiki majimbo 40 na kubakiza majimbo 14 ambayo hata leo yahakikiwa hadi kufikia saa nane mchana yatakuwa yatari na kutangazwa kwa matokeo hayo ambapo kesho kumuapisha rais huyo mpya asubuhi na baadaye kuenda dodoma kwenye kuhutubia bunge la jamhuri wa muungano wa Tanzania”amesema Profesa Lipumba.

Profesa Lipumba amesema kuwa uchaguzi huo ulifutwa baada ya kushindwa kwa dhahiri mgombea wa kiti hicho kupitia Chama cha Mapinduzi CCM ndipo hapo vyombo vya dola vikamshinikiza ambapo mwenyekiti watume hiyo alichukua hatua ya kuvunja katiba kwa kufuta uchaguzi huo

Prof. Lipumba amesema kuwa, hulka ya Chama Cha Mapinduuzi (CCM) kuingilia na kuvuruga matokeo sio mara ya kwanza na kwamba walianza mwaka 1995 akitoa mfano Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho kuwa aliiandikia barua tume kufuta uchaguzi na agizo hilo kutekelezwa.

error: Content is protected !!