April 14, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Prof. Lipumba aichambua Ripoti ya Hali ya Uchumi

Spread the love

PROFESA Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa CUF, ameichambua Ripoti ya Serikali ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa mwaka 2018, akisema kwamba baadhi ya takwimu zilizoanishwa katika ripoti hiyo haziendani na hali halisi. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Prof. Lipumba ameeleza hayo leo tarehe 22 Juni 2019 katika Kongamano la Sauti ya Haki na Furaha kwa Wote lililoandaliwa na CUF na kufanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Jijini Dar es Salaam.

Prof. Lipumba amesema  takwimu kuhusu ukuaji wa pato la taifa na la mwananchi haziendani na hali halisi ya uchumi wa nchi na wananchi, kutokana kwamba bado maisha ya Watanzania ni magumu na mazingira ya biashara kudorola.

“Hali yetu ya maisha hivi sasa imekuwa ni ngumu, wananchi wanalalamika wanasema vyuma vimekaza, ukisoma takwimu unaona takwimu nzuri. Lakini wafanyabiashara wanasema biashara haitoki. Moja ya tatizo mzungumko wa fedha katika uchumi umepungua,” amesema Prof. Lipumba.

Prof. Lipumba amesema kinachosababisha ugumu wa maisha ni ukosefu wa mazingira mazuri ya biashara pamoja na sera mbaya ya fedha zilizopelekea kudumaa kwa ukuaji uchumi na ujazi wa fedha.

“Ujazi wa fedha mwaka 2015 ulikuwa kwenye asilimia 14.5,  2016 ukapungua ukawa chini ya 1%, mwaka unaofuata ukawa kama 1.3%, mwaka jana ukawa chini ya 1%. Kwa wastani miaka mitatu iliyopita tokea 2016-2018 ujazi wa fedha za msingi, ukuaji wake uko chini ya 1%. Wakati hatuna tatizo la mfumuko wa bei,” amesema Prof. Lipumba na kuongeza.

 “Lazima patakuwa na tatizo katika mzungumko wa fedha. Utekelezaji wa sera yake ni nyepesi ni kiasi cha serikali iamue kukopa Benki Kuu, ujazi wa fedha utaongezeka.  Hili inawezekana.”

Kufuatia changamoto hizo, Prof. Lipumba ameishauri serikali kuziimarisha sekta binafsi, kuboresha sekta ya kilimo pamoja na kuwekeza katika nguvu kazi ya Watanzania.

“Ili kutoka tulipo lazima kuwekeza kwenye kilimo na viwanda. Lakini majukumu ya serikali ni kuwekeza kwenye nguvu kazi ya wananchi na kujenga mazingira ya sekta binafsi kuwekeza kwenye shughuli za biashara,” amesema Prof. Lipumba.

error: Content is protected !!