PROFESA Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), anahojiwa na Jeshi la Polisi mkoani Tanga kwa madai ya kufanya ziara bila kibali. Anaripoti Mwandishi Wetu, Tanga…(endelea).
Kiongozi huyo wa CUF, amekamtwa leo tarehe 26 Januari 2020, akiwa katika Kijiji cha Segera, wilayani Handeni kwa madai ya kuingia kwenye wilaya hiyo na kufanya shughuli za kisiasa bila kubali cha polisi.
Prof. Lipumba amekamatwa akiwa kwenye maandalizi ya kufungua tawi la chama hicho ‘Segera’. Baada ya kukamatwa, alipelekwa katika kituo kikuu wilayani humo kwa mahojiano zaidi.
Kukamatwa kwa kiongozi huyu kunathibitishwa na Masoud Mhina, Mkurugenzi wa Usalama wa chama hicho ambapo amesema ‘si kweli kwamba polisi hawakuwa na taarifa.’
Muhina amesema, CUF ilifuata utaratibu kwa kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi wilayani humo, na kwamba anashangaa hatua ya kukamatwa kwa mwenyekiti wa chama hicho.
Prof. Lipumba alikuwa akifanya ziara ikiwa leo ni siku ya mwisho, baada ya kuanza ziara hiyo wiki moja iliyopita mkoani humo.
Leave a comment