July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Prof. Lipumba ahoji uateuzi wa Prof. Muhongo

Spread the love

ALIYEKUWA mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba ametilia shaka uteuzi wa profesa Sosipeter Muhungo kwenye baraza jipya la mawaziri. Anaandika Faki Sosi…(endelea).

Amesema hayo kwenye mahojiano maalimu katika Kituo cha televisheni cha Azam Two, amesema kuwa waziri huyo mpya tayari ana tope la kashfa ya ufisadi wa ubadhirifu wa fedha kwenye akaunti ya Tegeta Escrow.

Amesema kuwa kashfa hiyo aliyoipata wakati wa awamu iliyopita imemfanya kukosa imani mbele ya watanzania walio wengi pande zote za nchi.

Sosipeter Mhongo ameteuliwa na kuapishwa kwenye wizara ya Nishati na Madini iliyohusishwa na ufisadi uliomhusisha yeye pamoja na Katibu Mkuu wa wizara hiyo.

error: Content is protected !!