Saturday , 22 June 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Prof. Kitila aongoza Ubungo, Dk. Tizeba na Shigongo ngoma droo
Habari za Siasa

Prof. Kitila aongoza Ubungo, Dk. Tizeba na Shigongo ngoma droo

Prof. Kitila Mkumbo
Spread the love

PROFESA Kitila Mkumbo, aliyekuwa katibu mkuu wizara ya Maji, ameshinda kura za maoni, kugombea Ubunge Jimbo la Ubungo, Dar es Salaam. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Leo Jumatatu tarehe 20 Julai 2020, Prof. Mkumbo amependekezwa kwa kura 172 kati ya kura 375, zilizopigwa na wajumbe wa mkutano mkuu Jimbo la Ubungo.

Wagombea katika kinyang’anyiro hicho walikuwa 110.

Akitangaza matokeo hayo, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana CCM (UVCCM), Dar es Salaam, Musa kilakala, Msimamizi wa Kura za Maoni Jimbo la Ubungo, amesema Prof.  Kitila ameoendekezwa kwa kura 172.

Mwanasiasa huyo alichuana na watia nia 109 akiwemo Mwantum Mgonja, Katibu Msaidizi Idara ya Siasa, Uhusiano wa Kimataifa CCM Bara aliyepata kura 73. Na Shamsa Mwangunga, aliyewahi kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii (Kura 9). Tatu Mapunda (11).

Kabla ya kujiunga na CCM,  Prof. Mkumbo alikuwa Mshauri wa Chama cha ACT-Wazalendo.

Kwa mujibu wa ratiba ya CCM, baada ya kura za maoni, tarehe 30 Julai 2020 Kamati za Siasa za Jimbo zinafanya vikao vya kuwajadili watia nia waliopendekezwa na Mkutano Mkuu wa Majimbo. Kisha kupeleka mapendekezo yake kwa Kamati za Siasa za Wilaya.

Tarehe 1 hadi 2 Agosti 2020, Kamati za Siasa za Wilaya zinaketi kujadili wagombea na kutoa mapendekezo yake kwa Kamati za Siasa za Mikoa. Ambazo zitaketi tarehe 4 hadi 5 Agosti 2020.

Kisha, Kamati za Siasa za Mikoa kisha zitatoa mapendekezo yake kwa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa (NEC) kwa ajili ya uamuzi wa mwisho.

Katika Jimbo la Buchosa Mkoa wa Mwanza, Mbunge anayemaliza muda wake, Dk. Charles Tizeba amefungana na mfanyabiashara maarufu nchini, Erick Shigongo kwa kupata kura 354 kila mmoja kati ya kura 751 zilizopigwa. Wagombea walikuwa 34.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali yaahidi kushirikiana na Prof. Ndakidemi kuhamasisha zao la kahawa

Spread the loveSerikali imeahidi kuungana na Mbunge wa Moshi Vijijini, Profesa Patrick...

BiasharaHabari MchanganyikoHabari za Siasa

IMF yaimwagia Tanzania trilioni 2.4 kukabili mabadiliko ya hali ya hewa

Spread the loveShirika la Kimataifa la Fedha (IMF) jana Alhamisi limesema bodi...

Habari za SiasaKimataifa

Mmoja afariki, 30 wajeruhiwa maandamano Kenya

Spread the loveMtu mmoja ameripotiwa kuuawa na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Nape awaomba wadau wa habari wamuamini

Spread the loveWAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye...

error: Content is protected !!