Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Prof. Kabudi: Tunatuhumiwa ukiukwaji haki za binadamu
Habari za Siasa

Prof. Kabudi: Tunatuhumiwa ukiukwaji haki za binadamu

Prof. Palamagamba Kabudi, Waziri wa Katiba na Sheria
Spread the love

TANZANIA inatuhumiwa kwa ukiukwaji wa haki za binadamu ikiwemo kujieleza, kutoa maoni, kujumuika na kukusanyika. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Akizungumza wakati wa uwasilishwaji wa Bajeti ya Wizaya ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa mwaka wa fedha 2020/21 leo tarehe 13 Mei 2020, Prof. Palamagamba Kabudi amesema, maeneo mengine Tanzania ‘inashambuliwa’ ni pamoja na marekebisho ya sheria zake ilizofanya chini ya utawala wa Rais John Magufuli.

“Tuhuma hizo zinahusishwa na marekebisho ya baadhi ya sheria zetu ambazo ni Sheria ya Vyombo vya Habari ya Mwaka 2016; Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta ya Mwaka 2018.

“…Sheria ya Vyama vya Siasa ya Mwaka 2018; Sheria ya Takwimu ya Mwaka 2018 na Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ya Mwaka 2019. 83,” amesema.

Hata hivyo, amelieleza Bunge kwamba tuhuma hizo hazina ukweli wowote na kwamba, zina nia ovu kwa kuwa Tanzania imepiga hatua kubwa katika kujiletea maendeleo.

“Naomba kulitaarifu Bunge lako Tukufu kuwa, tuhuma hizo hazina ukweli wowote,…Tuhuma zinazotolewa hutokana na uwepo wa tofauti za kimtazamo baina yetu na nchi au taasisi zinazotoa tuhuma hizo,” amesema.

Amesema, serikali inayoongozwa na Rais Magufuli inatambua na kuheshimu, wajibu wake Kikatiba na Mikataba ya Kimataifa ya kulinda na kudumisha haki zote za binadamu ikiwemo za kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiutamaduni.

Amesema, katika jitihada za serikali kuufahamisha ulimwengu namna inavyotetea na kusimamia haki za binadamu hapa nchini, Februari 2020, aliongoza ujumbe wa Tanzania kwenye Kikao cha 43 cha Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu.

“Kwenye kikao hicho, nilieleza kuhusu mafanikio ya serikali katika kulinda na kusimamia haki za elimu, afya, upatikanaji wa maji safi na salama, umeme na maendeleo ya kiuchumi.

“Nilielezea mafanikio yaliyopatikana katika kuongeza uwajibikaji kwa watumishi na viongozi wa umma; kupambana na vitendo vya rushwa; vita dhidi ya biashara ya dawa za kulevya; kuongezeka kwa kiwango cha ukusanyaji kodi; na kupanua wigo wa vyanzo vya mapato ili kuwahudumia wananchi wetu ipasavyo.”

Prof. Kabudi amesema, kufuatia ufafanuzi wa mara kwa mara kuhusu tuhuma hizo kwenye Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu, Jumuiya ya Kimataifa imeanza kutambua mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Tano katika kulinda na kusimamia haki za binadamu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!