July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Prof. Kabudi, Dk. Mpango washikwa pabaya

Dk. Philip Mpango, Waziri wa Fedha na Mipango

Spread the love

WITO kwa mawaziri wawili wa Rais John Magufuli; Prof. Palamagamba Kabudi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki naDk. Philip Mpango, Waziri wa Fedha na Mipango kutakiwa kujiuzulu, umeibuka tena bungeni. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Mawaziri hao jana tarehe 17 Juni 2019, walitakiwa kujiuzulu kwa madai ya kushindwa kumshauri vizuri Rais Magufuli katika kuinua uchumi wa nchi hivyo kusababisha kuliingiza taifa kwenye mkwamo.

Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini aliibuka na hoja hiyo wakati wa Mjadala wa Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/20. Mbunge huyo alisema kuwa, mawaziri hao wawili wameshindwa kuwa msaada mkubwa katika masuala ya fedha na uchumi kwa rais wa nchi.

Akichangia mjadala huo Msigwa alisema, tangu serikali ya awamu ya tano iingie madarakani, kambi kuu ya upinzani imekuwa ikiishauri serikali katika mambo mbalimbali ya kiuchumu, lakini mawaziri hao wameshindwa kubeba mawazo hayo na kumshauri Rais Magufuli na hivyo nchi kuyumba kiuchumi.

“Tangu mwaka 2016, tumekuwa tukiishauri serikali katika masuala ya uchumi,” amesema Msigwa na kwamba, Dk. Mpango na Prof. Kabudi wameshindwa kutoa ushauri huo huku wakimshauri vibaya Rais Magufuli.

‘Ni miaka mine sasa hapa bungeni tumekuwa tukijadili maendeleo yetu kuhusu bandari, masuala ya utalii na kukusanya kodi pia. Leo baada ya miaka mine mmebadili lugha na kuwa laini,” amesema Msigwa akiongeza kuwa, masuala yanayofanyika sasa kuhusu uchumi wa nchi na mapato ya serikali, yalishauriwa miaka mine iliyopita.

“Ule ushauri tuliowapa wakati hule na mkaukataa, kwani mlikuwa mnataka nini?” amehoji Msigwa na kuongeza “baada ya kuliingiza taifa kwenye matatizo, sasa mnatekeleza yale yale.”

Ametaja moja ya sababu zinazoashiria Dk. Mpango kushindwa kazi, ni pamoja na wasaidizi wake wakiwemo makamishna mbalimbali wa taasisi zilizo chini ya wizara yake kuondolewa.

error: Content is protected !!