Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Prof. Kabudi: Afrika hakuna kama Mwl. Nyerere
Habari za Siasa

Prof. Kabudi: Afrika hakuna kama Mwl. Nyerere

Spread the love

WAZIRI wa Mambo ya Nje ya Nchi, Prof. Palamagamba Kabudi amesema, hakuna kiongozi aliyefanya makubwa Afrika zaidi ya Rais wa Awamu ya Kwanza, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Anaripoti Hamis Mguta … (endelea).

Kabudi ametoa kauli hiyo leo tarehe 21 Agosti 2019, wakati akitoa shukrani kwa waandishi wa habari kutokana na ushiriki wao katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).

Amesema, miongoni mwa viongozi ambao waliwahi kusema hadharani kuwa kiongozi huyo ni mkubwa kuliko wote ni Rais wa Uganda, Yowel Kaguta Museveni.

“Katika nyakati hizi, hakuna kiongozi mkubwa wa Bara la Afrika zaidi ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, hakuna nchi yoyote iliyo kusini ambayo haikusaidiwa na Tanzania kupata Uhuru au kujitegemea,” amesema.

Ameeleza, moja ya sababu ambayo ameitoa Rais wa Afrika Kusini, Matamela Cyril Ramaphosa kuhusu maendeleo ya Tanzania alipokwenda mkoani Morogoro kwa jailli ya ziara ya kutembelea makaburi ya mashujaa waliopigania uhuru wa nchi hiyo, ni kuwa maendeleo yanayoonekana sasa Tanzania, yamechelewa kwasababu ya kusaidia nchi zingine kwa kutumia rasilimali zake.

“Rais Ramaphosa alisema, kule mazimbu kwamba Tanzania ilifika hatua ya kubomoa madaraja yake na kuharibu barabara zake ili Wareno wasivamie nchi hiyo.

“Sehemu mbalimbali za Tanzania ni mahala viongozi wengi wa Afrika wamepata mafunzo yao,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Chadema: Samia aunde tume kuchunguza mauaji mgodi wa Barick

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameombwa aunde tume huru kwa...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

error: Content is protected !!