January 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Prof. Baregu: Tupo tayari kuendesha nchi

Marehemu Profesa Mwesiga Baregu

Spread the love

MWENYEKITI wa jopo la washauri wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Prof. Mwesiga Baregu amesema wamejiandaa kuunda serikali mpya mara tu watakapoingia madarakani. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Prof. Baregu ametoa kauli hiyo leo Jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amewaambia, uhakika wa kupata ushindi unatokana na utafiti walioufanya kutoka kwa wananchi ndani ya kipindi hiki cha kampeni.

“Tunauhakika wa kukubalika na wananchi wengi kwani kampeni zetu tulizifanya kwa kistaarabu, bila matusi, kejeri wala kupiga pushap.

“Licha ya kutukanwa na kuchokozwa, hatukuvunja heshima yetu kwani tuna uhakika wa rais wetu na ushindi tunapata,” amesema Prof. Baregu.

Kuhusu uteuzi wa mawakala, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Regnald Munisi amesema kuwa, “mikoa yote mawakala wameteuliwa na tunauhakika nao.

“Tumewachuja, na tumewaamini kuwa watatufaa kwani ni watu ambao ni wazalendo, wamepigania haki kwa miaka mingi kwa hiyo ni watu ambao haitakuwa rahisi kupewa rushwa kwani wana mapenzi ya dhati na chama,” anesema Munisi.

Munisi wakati akiunga hoja ya Prof. Baregu pia amesema, ili kuepusha “bao la mkono” kutokea wameandaa kituo maalumu cha kupokea matokeo kutoka kwa mawakala wa kila eneo ili na wao wapate muda wa kujumlisha na kupata idadi ya kura za ukweli.

Amesema, kituo hicho kimeunganishwa na mitambo maalumu itakayokuwa inatumia data ili kupokea data, picha na matukio yote yatakayo kuwa yanatokeo vituoni.

“Tumeshawaandaa vijana wapatao 800 kwa ajili ya kazi hiyo, ambapo watakuwa wakizambaza na tokeo tutakayokuwa tunayapata kwa njia za mitandao ili kuweza kumfikia kila mmoja kwa wakati na usahihi.

“Endapo matokeo yetu yatatofautiana na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), itabidi tukae watueleze vizuri.” amesema Munisi.

Mbali na hilo, Munisi amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kesho katika mkutano wa kufungia kampeni utakaofanyika katika Uwanja wa Jagwani kuanzia sa 5 asubuhi hadi saa 9 mchana ambapo viongozi wote wa Ukawa watakuwepo.

error: Content is protected !!