Saturday , 3 June 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Prof. Assad awekwa kando, Spika Ndugai kupumua?
Habari za SiasaTangulizi

Prof. Assad awekwa kando, Spika Ndugai kupumua?

Prof. Mussa Assad, Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali. Picha ndogo Job Ndugai, Spika wa Bunge
Spread the love

PROFESA Mussa Assad, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), amewekwa kando na sasa Charles Kichere ameteuliwa kuchukua nafasi hiyo. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Taarifa kutoka Kurugenzi ya Mawasiliano Ikule leo tarehe 3 Novemba 2011, imeeleza kwamba Prof. Assad amemaliza kipindi chake cha miaka mitano kuhudumu kama CAG.

Kwenye taarifa hiyo iliyosainia na Gerson Msigwa, Mkuu wa Mawasiliano Ikulu, uteuzi huo imetangazwa na Balozi John Kijazi, Katibu Mkuu Kiongozi.

Balozi Kijazi ameeleza, ukomo wa Prof. Assad kama CAG unahitimishwa tarehe 4 Novemba 2019. Kabla ya uteuzi huo, Kichere alikuwa Katibu Tawala mkoani Njombe, pia aliwahi kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Je, Job Ndugai, Spika wa Bunge amepumua?

Prof. Assad na Spika Ndugai wameingia kwenye msuguano kuanzia mwishoni mwa mwaka jana, baada ya Prof. Assad kusema ‘Bunge ni dhaifu’ alipokuwa nje ya nchi.

Bunge lilitangaza azimio la kutofanya kazi na Prof. Assad, lilipitisha azimio hilo baada ya kumtuhumu kudharau chombo hicho na baadaye kumtia hatiani.

Prof. Assad alitiwa hatiani na Bunge baada ya kumtuhumu kulidhalilisha kufuatia kauli yake aliyoitoa katika mahojiano yake na Idhaa ya Kiswahili ya Redio ya Umoja wa Mataifa (UN), jijini New York nchini Marekani, Desemba mwaka 2018.

Katika mahojiano hayo na kituo hicho cha radio ya umoja wa mataifa, Prof. Assad alisema, Bunge la Tanzania halina meno na hivyo limeshindwa kuiwajibisha ipasavyo serikali.

Aidha, Prof. Assad aliwahi kuliambia Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), kwamba “sina maamuzi ya kufanya zaidi ya kuomba dua watu waongoze vizuri na wafanye maamuzi yenye faida na nchi hii. Hilo ndilo ninaloweza kulifanya kwa sasa.”

Alikuwa akijibu swali la mtangazaji wa kituo hicho aliyetaka kujua kama anaweza kuchukua “maamuzi magumu ya kuachia ngazi.

Alisema, “…kama tunatoa ripoti na inaonekana kuna ubadhilifu, halafu hatua hazichukuliwi, huo kwangu mimi ni udhaifu. Bunge linatakiwa liisimamie serikali na kuhakikisha kuwa pahali penye matatizo basi hatua zinachukuliwa.

“Sisi kazi yetu ni kutoa ripoti tu; na huo udhaifu nafikiri ni jambo la kusikitisha, lakini ni jambo tunaamini muda si mrefu huenda likarekebishika.

“Tunadhani tatizo kubwa linatokana na Bunge kushindwa kufanya kazi yake kama linavyotakiwa,” alieleza Prof. Assad katika mahojiano yake na Radio ya UN.

Mara baada ya Ndugai kuongoza Bunge na kupitisha azimio hilo, wananchi waliowengi wameonekana kumuunga mkono Prof. Assad na wengine kufika mbali zaidi kwa kumtaka Spika kuachia ngazi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Bosi NIC apandishwa kizimbani, akabiliwa na mashitaka 365

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bima la Taifa...

Habari za Siasa

Lusinde: CCM hatuliachii ng’o jimbo la Moshi Mjini

Spread the loveMJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Livingston...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar: Bakharesa hajavamia shamba letu

Spread the love  IKULU Visiwani Zanzibar, imeeleza kuwa eneo la kiwanda cha...

Habari za SiasaTangulizi

Zanzibar watangaza rasmi kuwa shamba la Razaba ni mali yao

Spread the love  SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), imetangaza rasmi kwamba shamba...

error: Content is protected !!