Saturday , 9 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Prof. Assad aibuka, aacha maswali
Habari za SiasaTangulizi

Prof. Assad aibuka, aacha maswali

Spread the love

ALIYEKUWA Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Tanzania (CAG), Prof. Mussa Assad, amekana madai kuwa alitekwa na genge lililopachikwa jina la “watu wasiojulika.” Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea). 

Jana tarehe 25 Desemba 2019 (Jumatano), taarifa zilisambaza kupitia mitandao ya kijamii zikisema, Prof. Assad ametekwa na watu wasiojulikana na hata familia yake, haifahamu mahali aliko.

Miongoni mwa watu waliokuwa wakisambaza taarifa hizo, ni mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Zuberi Kabwe na mwanaharakati mashuhuri kwa njia ya mitandao ya kijamii, anayefahamika kwa jina la Kigogo 2014.

Akizungumza na baadhi ya mwandishi wa habari hizi leo Alhamisi, tarehe 26 Desemba, nyumbani kwake jijini Dar es Salaam, Prof. Assad alikana madai hayo ya kutekwa na kuongeza, “kama kuna watu wanadhani, kuna mambo hayako sawa, ni vizuri wakayazungumza.”

Alisema, “mimi nadhani kuna mambo ambayo hayazungumzwi; ndio maana hisia kama hizi za kutekwa hujitokeza. Nawashauri Watanzania kama wanaona kuna mambo hayako sawa wayaseme. Ulinzi wa katiba ya taifa letu, ni kazi ya kila mmoja wetu….”

Akizungumza kwa kujiamini, Prof. Assad amesema, hakutekwa na kwamba mambo yote yanayuhusu maisha yake amemuachia Mungu.

“Sijatekwa. Nilikuwa kwenye warsha ya siku tatu wilayani Kisarawe mkoani Pwani, ambayo iliandaliwa na Umoja wa Wanataaluma wa Kiislamu Tanzania (TAMPRO), iliyokuwa na lengo la kuhuisha taasisi hiyo,” ameeleza Prof. Assad na kuongeza:

“Eneo nililokuwa halikuwa na mtandao wa simu. Nilimuaga mke wangu na niliondoka kwa kutumia gari yake aina ya GD Wagon mpaka Kisarawe ambako mimi nilifanya kazi kwa siku moja.” 

Anasema, alifika Kisarawe saa mbili asubuhi na alianza safari ya kurejea nyumbani kuanzia saa tatu usiku.

Anasema, simu zake zilianza kuingia alipofika Kisarawe na kwamba yeye amejiwekea utamaduni wa kutopokea simu wakati akiwa anaendesha gari.

Prof. Assad anasimulia kuwa hakupokea simu mpaka alipofika Ukonga, ambako aliona simu ya kijana wake ambaye alimwambia yuko barabarani na kijana wake akamjibu kuwa “basi inatosha ngoja niwaeleze nyumbani.”

Akijibu swali kwa nini anadani watu walikuwa wana wasiwasi kuwa si wanafikiri kuwa alitekwa, Prof. Assad anasema, kama kuna watu wanadhani kuna jambo halikufanywa sawasawa waliseme, ili wanaofanya maamuzi wafahamu kuwa jambo fulani halikufanywa vizuri. 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mbowe: Miaka 62 ya uhuru tujenge upya mioyo yetu

Spread the loveWAKATI Tanganyika ikiadhimisha miaka 62 tangu kupata uhuru, Mwenyekiti wa...

Habari za Siasa

Rais Samia asamehe wafungwa 2,244

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewasamehe wafungwa 2,244, huku akiwabadilishia...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataka jamii inayohoji mafisadi

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan ametoa maagizo juu ya uboreshaji dira...

Habari za SiasaTangulizi

Kapinga: Kukatika kwa umeme siyo hujuma

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga amesema Serikali ipo kazini...

error: Content is protected !!