July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

PRO: Simu zinaingizwa magerezani

Wafungwa wakishona nguo za wafungwa katika kiwanda cha nguo kilichopo katika Gereza la Ukonga

Spread the love

MKUU wa Magereza Mkoa wa Dar es Salaam (RPO), Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP), Joel Bukuku, amekiri baadhi ya wafungwa kushirikiana na askari magereza wasio waadilifu, kuiingiza simu magerezani, jambo ambalo ni kinyume na utaratibu. Anaandika Edson Kamukara…(endelea)

ACP Bukuku alikiri hali hiyo, wakati akihojiwa na baadhi ya waandishi wa habari ofisini kwake katika hitimisho la ziara yao ya kutembelea magereza kadhaa mikoani kwa lengo la kujifunza utekelezaji wa programu ya urekebishaji wafungwa kupitia miradi inayoendeshwa na jeshi hilo.

Amesema ni kosa kwa mfungwa kuingiza simu gerezani na kwamba wanapowabaini hatua kali zinachukuliwa pamoja na askari jela wanaokuwa wameshirikiana nao.

“Ni kweli simu zinaingizwa magerezani na wafungwa kwa kificho au kwa kula njama na askari wasiokuwa waadilifu. Hili ni kosa kwa mujibu wa sheria zetu za magereza, hivyo tunapobaini hatua kali zinachukuliwa kwa aliyehusika.

“Hili ni suala ambalo linafanyika kwa kificho sana. Kwa mfano mdogo tu, hivi karibuni kuna mfungwa wa kike tulimbaini ameficha simu kwenye sehemu zake za siri (ukeni) hadi tukalazimika kumpatia huduma ya kumlaza kuweza kuitoa,” amesema.

ACP Bukuku ameongeza kuwa pamoja na usiri huo unaotumika, bado wameendelea kupiga vita hali hiyo kwa kuwaeleimisha wafungwa kujiepusha na vitu visivyoruhusiwa kuingizwa magerezani.

Kuhusu msongamano wa wafungwa, ACP Bukuku amesema kuwa magereza manne ya mkoa wa Dar es Salaam ya Ukonga, Segerea, Geraza la mahabusu Keko na Wazo Hill miundombinu yake imechakaa na hivyo kuelemewa na idadi ya wahalifu.

“Gereza la Ukonga ndilo kubwa na kongwe lililoanzishwa mwaka 1952 likiwa na uwezo wa kuhifadhi wahalifu 1500. Keko lilianzishwa mwaka 1957 likiwa na uwezo wa kuchukua wahalifu 340 lakini sasa linao 1000 hadi 1200 huku Segerea lililoanzishwa mwaka 1991 likiwa na uwezo wa kuchukua wahalifu 1200, hivi sasa linanao 1700 hadi 2000.

error: Content is protected !!