July 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Prince Charles, Camilla kuhudhuria mkutano wa Jumuiya ya Madola Rwanda

Spread the love

 

MWANAMFALME wa Wales na Duchess wa Cornwall, wamewasili nchini Rwanda katika mji mkuu wa Kigali siku ya Jumanne usiku , kabla ya mkutano wa kilele wa viongozi wa Jumuiya ya Madola. Anaripoti Rhoda Kanuti kwa msaada wa Mashirika ya Kimataifa.

Haya yamejiri baada ya kuripotiwa kuwa mwanamfalme huyo, alikosoa kwa siri mpango wa Uingereza kwa kutuma waomba hifadhi nchini Rwanda.

Kulingana na madai yaliyoripotiwa na gazeti la Times mapema mwezi huu,mrithi wa kiti cha ufalme alisemekana kuamini kuwa sera hiyo, ilikuwa ya kutisha.

Aidha Prince Charles amekwenda kumuwakilisha Malkia wa Jumuiya ya Madola katika hafla hiyo, ambayo iliahirishwa mwaka 2021 mpaka 2020 kwasababu ya janga la corona

Lakini safari hiyo, ya kwanza ya ndege iliyopaswa kuchukua waomba hifadhi kutoka Uingereza hadi Rwanda ilisitishwa wki iliyopita , dakika chache ya ndege kupaa kufuatia maamuzi ya kisheria ya mahakama ya haki za binadamu ya Ulaya.

Pia katika ziara hiyo mrithi wa kiti cha ufalme atakutana na manusura , wahusika wa mauaji ya kimbari ya Rwanda.

error: Content is protected !!