January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

PPRA yaomba usaidizi wa wanahabari

Waziri wa Afya Dorothy Mwanyika

Spread the love

NAIBU Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Dorothy Mwanyika, amewataka waandishi wa habari kusaidia kuelimisha jamii itambue umuhimu wa sheria ya manunuzi ya umma ya mwaka 2004, ambayo iliendelea kufanyiwa marekebisho, na kanuni zake za mwaka 2013, ili kuwezesha fedha za bajeti ya Serikali kutumika vizuri. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Mwanyika alitoa wito huo, wakati akifungua warsha ya elimu ya manunuzi ya umma kwa wadau wa habari nchini, ambayo imeandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Ununuzi  wa Umma (PPRA) na kushirikisha wahariri na waandishi kutoka mikoa mbalimbali.

Amewataka wahariri na wanahabari kutumia nafasi zao kuhakikisha jamii inapata uelewa wa kutosha kuhusu PPRA.

“Waandishi wanatakiwa kutumia taaluma zao katika kuibua na kuripoti habari hususani changamoto zinazoikabili sekta hii, zikiwemo vitendo vya rushwa, ubadhirifu, malipo hewa pamoja na miradi mingi kutekelezwa chini ya viwango.

“Hakika mkifanya hivyo, mtakuwa mmechangia kwa kiasi kikubwa kuokoa kiasi kikubwa cha fedha za walipa kodi ambao ni wananchi. Asilimia 70 ya fedha za Serikali matumizi ya kawaida pamoja na fedha za maendeleo zinatumika  kununua huduma na bidhaa,” amesema.

Mwanyika pia, amewapongeza wanahabari kwa kuendelea kuhabarisha umma juu ya masuala ya maendeleo na changamoto mbalimbali zinazowakabili PPRA.

Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA, Dk. Laurent Shirima, amesema  kumekuwa na malalamiko mengi juu ya utendaji wa PPRA, huku wengine wakidai kuwa sheria na kanuni zilizowekwa hazifai kwa kuwa zinaongeza gharama wakati wa kufanya manunuzi.

“Ukweli ni kwamba, sheria si ngumu, ila tu wananchi wengi wanauelewa mdogo kuhusu sekta hii, ndio maana tumewaita wanahabari kwani mkielewa mtasaidia kuelimisha jamii,” amesema Shirima.

error: Content is protected !!