November 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Poulsen akubali mziki wa Congo

Kim Poulsen Kocha wa Taifa Stars

Spread the love

 

MARA baaada ya kupoteza mchezo kwa bao 3-0, dhidi ya Timu ya Taifa ya Jamhuri ya Congo, kocha wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Kim Poulsena amekili kupoteza mchezo huo, mbele ya timu bora. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Mchezo huo wa kundi J, kufuzu fainali za kombe la Dunia Qatar 2022, ulipigwa jana kwenye dimba la Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam na kuhudhuliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa.

Akizungumza na wanahabari mara baada ya mchezo huo kumalizika, Poulsen alisema kuwa wapinzani wao Congo ni moja ya timu ngumu na yenye uozefu kwenye michuano hiyo.

“Congo ni Timu ngumu na yenye uzoefu na tumepoteza mchezo wa leo (jana) kutokana na makosa ya wachezaji binafsi.” Alisema Poulsen

Kipigo cha Taifa Stars kwenye mchezo huo kilifuta ndoto ya kufuzu kwa hatua inayofuata kwenye michuano hiyo, kutokana na umuhimu wa ushindi kwenye mchezo huo.

Aidha kocha huyo aliendelea kufunguka kuwa, unaweza kuadhibiwa kama ukifanya makossa mbele ya timu iliyowazidi viawango vya ubora vya Shirikisho la Mpira wa Miguu Dunia.

“Unaweza kufungwa kama ukifanya makosa kwa timu iliyowazidi viwango vya ubora vya shirikisho la mpira wa Miguu Dunia (FIFA), kila kosa utaadhibiwa.”  Alimalizia kocha huyo

Katika hatua nyingine Poulsen aliwaomba radhi watanzania kwa kupoteza mchezo huo, kwa kuwa walikuwa na matarajio makubwa. Huku akisema bila kusita kuwa amepoteza mchezo huo mbele ya timu iliyoewazidi viwango.

“Naomba radhi kwa kufungwa leo (jana) kwa sababu tulikuwa na matarijio makubwa, tulifanya makosa baada ya dakika sita na tukaadhibiwa.”

Stars itasafiri leo jioni kuelekea nchini Madagascar kwa ajili ya mchezo wa kukamilisha ratiba utakaopigwa tarehe 14, Novemba 2021, jijini Antananarivo.

Mabao ya Congo kwenye mchezo wa jana yalifungwa na Kakuta dakika ya sita, Iduma Fasika kwenye dakika ya 66’ na bao la tatu liliwekwa kambani na Ben Malango kwenye dakika 85 ya mchezo.

error: Content is protected !!