May 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Poulsen aita 28 Stars, Kabwili ndani

Kim Poulsen, kocha wa Timu ya Taifa ya Tanzania

Spread the love

 

Kocha wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa stars) Kim poulsen ametangaza majina ya wachezaji 28 watakaoingia kambini kujiandaa na mashinadano ya  kuwania kufuzu fainali za kombe la Dunia litakalofanyika nchini  Qatar 2022. Anaripoti Mintanga Hunda/TUDARCo…(endelea)

Kikosi hicho kitaingia kambini Agosti 24, mwaka huu, huku akijumuishwa golikipa namba tatu wa klabu ya Yanga, Ramadhan Kabwili ambaye ni mara ya kwanza kuitwa kwenye timu ya wakubwa ya Taifa stars.

Stars itacheza michezo miwili ya kufuzu michuano hiyo kwenye kundi J, ambapo mchezo wa kwanza utapigwa ugenini Septemba 2, 2021, dhidi ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, majira ya saa 10 jioni kwenye Uwanja wa TP Mazembe, Lubumbashi.

Mchezo wa pili wa Stars kwenye kundi hilo, utakuwa dhidi ya Madagascar, septemba 7 2021, majira ya saa 10 kwenye dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Akitangza kikosi hiko hii leo Agosti 19, 2021 mbele ya waandishi wa Habari kwenye makao makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Kim alisema kuwa kwa sasa ameita wachezaji 28, watakaoingia kambini hivi karibuni, lakinbi wachezaji watakaosafiri watakuwa ni 23.

Ramadhan Kabwili

“Kwa sasa nimeita wachezaji 28 watakaoingia kambini, ila watakaosafiri ni wachezaji 23, nataka niende na idadi kubwa ili ikitokea changamoto yoyote kwa mchezaji basi tuwe na mbadala hasa kwenye upimaji wa virusi vya corona.” Alisema kocha huyo

Kikosi hiko kinatarajia kuondoka jijini Dar es Salaam Agosti 30, mwaka huu kuelekea nchini Congo kwenye mchezo huo wa kwanza kuwania kufuzu michuano ya kombe la Dunia.

Aidha Poulsen alinena kuwa kikosi hiko kinatakuwa na mchanganyiko wa wachezaji vijana ili kusaidia kuwakuza kuwa wachezaji wazuri.

“Unakumbuka Aishi Manula alikuwa mchezaji kwenye timu ya vijana, lakini kwa sasa ndio kipa namba moja, tunahitaji kuwakuza hawa ili waje kuwa wachezaji wazuri” alifunguka Paulsen

Wachezaji 28, ambao wameitwa kwenye kikosi hiko ni Aishi Manula,  Shomari Kapombe, Israel Mwenda, Erasto Nyoni, Mohamed Hussein, Kennedy Juma, John Bocco na Mzamiru Yassin wote kutoka Simba.

Wengine ni Ramadhani Kabwili, Dickson Job, Bakari Mwamnyeto, Zawadi Mauya na Feisal Salum wote kutoka klabu ya Yanga.

Kutoka klabu ya Azam FC Wilbol Maseke, Lusajo Mwaikenda, Abdulrazack Mohamed, Edward Manyama, Ayoub Lyanga, Mudathir Yahya, Salum Abubakar na Iddy Selemani.

Wengine ni Metacha MnataNickson Kibabage [Youssoufla FC-Morocco], Meshack Mwamita [Gwambina FC], Novat Dismas [Maccabi Tel Aviv-Israel], Abdul Hamis Seleman [Coastal Union], Mbwana Samatta [Fenerbahce-Uturuki] na Simon Msuva [Wydad Athletic-Morocco].

error: Content is protected !!