Friday , 29 September 2023
Home Kitengo Michezo Poulsen aita 25, Bocco na Mkude ndani
Michezo

Poulsen aita 25, Bocco na Mkude ndani

Spread the love

 

KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya Tanzania ‘Taifa Satrs’ Kim Poulsen amewaitaka kambini wachezaji 25 wawiwemo Jonas Mkude na John Bocco. Anaripoti Wiston Josia TUDARCo …  (endelea).

Bocco na Mkude ambao wote ni wachezaji wa Simba wamejumuishwa katika kikosi hicho kujiandaa na mchezo wa kufuzu kombe la dunia nchini Qatar mwaka 2022.

Ni baada ya kukosekana katika michezo miwili iliyopita dhidi ya Congo wa ugenini na ule uliopigwa nyumbani jijini Dar es Salaam, katika dimba la Benjamin Mkapa.

Katika michezo hiyo, Stars ilijikusanyia pointi nne, baada ya kutoka sare ya 1-1na Congo na kuibuka na ushindi dhidi ya Madagascar wa 3-2.

Stars itacheza na Benin katika dimba la Mkapa tarehe 7 Oktoba 2021 ambapo leo Jumatatu, tarehe 27 Septemba 2021, Poulsen ameitaja jeshi lake ambalo litaingia kambini 4 Oktoba.

Akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya Shirisho la Soka Tanzania (TFF), Poulsen amesema, suala la kuchagua wachezaji wa kucheza Timu ya Taifa anaangalia ubora katika klabu anayocheza.

Ametolea mfano, Yusufu Mhilu, aliyekuwa Kagera Sugar pamoja na Israel Patrick Mwenda, alikuwa KMC ambao baada ya kuitwa timu ya Taifa wamesainiwa timu kubwa ya Simba.

Akizungumzia kundi lake, kocha huyo amesema, wachezaji wa timu pinzani tulionao kwenye kundi moja asilimia 80 wanacheza Ulaya tofauti na “sisi ambao asilimia 90 wanacheza hapahapa nyumbani.”

Amewataja wachezaji aliowaita; ni Aishi Manula, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Kennedy Juma, Mohammed Hussein, Mzamiru Yassin, John Bocco na Jonas Mkude wote kutokea Simba.

Wengine ni, Ramadhani Kabwili, Dickson Job, Bakari Mwamnyeto na Feisal Salumu Abdalah ‘Fei Toto’ wote kutokea Yanga). Pia wamo, Wilbrod Maseke, Idd Nado Lusajo, Mwaikenda Edward Manyama wote wa Azam FC.

Pia wao, Nickson Kibabage (Kmc FC), Meshack Mwamita (Kagera Sugar), Abdul Suleiman (Coastal Union) na Reliant Lusajo (Namungo FC).

Wanaokipiga kimataifa waliotwa ni Simon Msuva (Wydad AC-Moroco) na nahodha wa kikosi hicho, Mbwana Sammata anayeichezea Royal Antwerp ya Ubelgiji.

1 Comment

  • Halo Kocha,
    Naomba unionyeshe timu za taifa za Amerika kusini na kaskazini, Ulaya na Asia zinazochukua zaidi ya wachezaji 3 kutoka timu moja. Lazima, ubadilishe na siyo kuita kwa mazoea.
    Kama unaweza kufundisha, huhitaji kutegemea wachezaji walewale.
    Hii ya Simba na Yanga kugeuza timu zingine mashamba ya bibi ni udhaifu wa TFF na viwanja kumilikiwa kisiasa. Timu tunazozifunga leo ni zile zile tumekuwa tukizifunga miaka 20 na ushee.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Meridianbet yaibukia Tandika, yafungua duka jipya

Spread the love BAADA ya kupita maeneo mbalimbali hatimae kampuni yaMeridianbet imeibukia...

BiasharaMichezo

Ukiwa na Meridianbet ni rahisi kuwa milionea

Spread the love  CARABAO Cup raundi ya 3 Uingereza inaendelea na mechi...

Michezo

Jezi ya Samatta iliyoifunga Liverpool kuuzwa Genk

Spread the love  KLABU ya KRC Genk ya nchini Ubelgiji imeamua kuanza...

BiasharaMichezo

Hii ndio historia ya El-Clasico, derby bora zaidi duniani

Spread the love  KILA nchi ina vilabu viwili hasimu na pinzani nje...

error: Content is protected !!