VUGUVUGU la madiwani wa upinzani kukimbilia Chama Cha Mapinduzi (CCM) halijapoa, jimboni Hai, Kilimanjaro katika Kata ya Kia, diwani wake amehamia chama tawala. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).
Timoth Laizer, ambaye alikuwa diwani wa kata hiyo kupitia Chadema sasa ni mwanachama wa CCM. Jimbo la Hai ndio linaongozwa na Freeman Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema Taifa.
Laizer leo tarehe Agosti 2, 2018 amesema kuwa, ameamua kuhama Chadema kwa sababu alizozitaja kuwa ni kutoridhishwa na maelekezo yanayotolewa na uongozi wa chama hicho yakutoshiriki wala kutotambua kazi ya maendeleo inayofanywa na Serikali ya CCM.
“Nimeamua kujiunga nha CCM chama pekee kilichobaki kuwatetea wanyonge katika nchi hii kutokana na ukweli kwamba siwezi kuendelea kuwa kwenye chama kinachotupa maelekezo ya kutoshiriki wala kuzitambua kazi zozote zinazofanywa na Serikali wakati kiuhalisia serikali ya Rais John Magufuli ndio iliyoweza kupambana na shida na dhiki za watanzania wanyonge ” amesema Laizer.
Leave a comment