October 2, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Pondamali afunguka safari ya Lagos 1980

Spread the love

MLINDA mlango wa zamani wa timu ya Taifa ya Tanzania, Juma Pondamali amesema kuwa safari ya timu hiyo kufuzu katika michuano ya lililokuwa kombe la mataifa huru ya Afrika mwaka 1980 haikuwa rahisi kwa kuwa walikutana na timu nyingi ngumu. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea)

Akizungumza katika mahojiano maalumu na MwanaHALISI TV, Pondamali amesema kuwa kundi waliopangiwa kwa ajili ya kusaka tiketi ya michuano hiyo lilikuwa na timu tano na ilihitajika kupita moja tu.

“Kipindi kile kulikuwa na timu kama Kenya (Harambee Star), Madagasca, Zambia, Tanzania na Mouritius , kundi lilikuwa na timu tano lakini hapo ilikuwa inapita timu moja, sasa kama ilikuwa hivyo basi makundi yetu yalikuwa magumu kuliko haya,” alisema Pondamali.

Golikipa huyo aliongezea kuwa hata walipoenda kwenye michuano hiyo Lagos walipangiwa kundi gumu kiasi cha kuhisi kama walionewa kwa kuwa kundi hilo lilikuwa na miamba ya soka wa Afrika kwa wakati huyo.

“Tunaweza kusema CAF walituonea maana huo mziki waliotuwekea ulikuwa hatari, kwa sababu tulipangiwa kundi moja na mwenyeji ambaye ni Nigeria, Misri na Ivory Coast. Tulihisi kama walituonea,” aliongezea Pondamali.

Pondamali ambaye kwa sasa ni kocha wa makipa wa klabu ya Yanga ambayo inashiriki Ligi Kuu Tanzania Bara na kuna muda alishawahi kuwa kocha wa makipa wa Taifa Stars.

Tazama mahojiano kamili hapo chini

 

error: Content is protected !!