Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari Polisi yazungumzia sakata la Nabii Mwingira
HabariTangulizi

Polisi yazungumzia sakata la Nabii Mwingira

Spread the love

 

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam nchini Tanzania limesema, linaendele na uchunguzi dhidi ya tuhuma mbalimbali zilizotolewa na Kiongozi wa Kanisa la Efatha, Mtume na Nabii Josephat Mwingira na kesho Alhamisi, tarehe 30 Desemba 2021, litatoa taarifa. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Uchunguzi huo unafanyika baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene kuliagiza jeshi hilo la polisi kumtafuta na kumhoji Nabii Mwingira anayetuhumiwa kutoa lugha nzito dhidi ya Serikali.

Baada ya agizo hilo la Waziri Simbachawene alilolitoa Jumatatu ya tarehe 27 Desemba 2021, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari alisema, tuhuma alizozitoa Nabii Mwingira, zinahitaji kuchunguzwa.

Alisema, “…tuhuma nzito sana na zinapotolewa na kiongozi ambaye ni wa kijamii katika dini na kiongozi maarufu anayejulikana, tunapata shida kidogo” na hazipaswa kuachwa bila kufanyiwa kazi hivyo “RPC wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, amtafute ili tuweze kupata maelezo yake zaidi.”

Mara baada ya taarifa hiyo, jioni ya siku hiyo hiyo, Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro alitoa saa 24 kwa Nabii Mwingira kujisalimisha ili kuweza kuhojiwa.

Leo Jumatano, MwanaHALISI Online limemtafuta kwa simu, Kamanda Muliro kujua kinachoendelea kuhusu Nabii Mwingira ambapo amesema, “tutatoa taarifa kesho na kwa sasa tuacheni tuendelee na uchungizi wetu.”

Jumapili ya tarehe 26 Desemba 2021, akiwa kanisani kwake, Mwenge jijini Dar es Salaam, Nabii Mwingira alitumia mahubiri kwa waumini waliojitokeza kwa wingi kutoa tuhuma mbalimbali ikiwemo kunusurika kuuawa na watu wa serikali.

Miongoni mwa tuhuma hizo, Nabii Mwingira alielezea jinsi, dereva wake aliyehusishwa katika mauaji na baada ya kugundua alimpokonya simu huku dada aliteyetoa taarifa za mipango ya kuuawa kwake “aliuawa Rombo Hotel Shekilango Dar es Salaaam.”

Nabii Mwingira alisema, “kama mtu una Mungu unakimbia nini, mimi nikimbie Tanzania kwa sababu wanataka kuniua, siende popote na kama bwana anataka nife nitafia hapa.”

Huku waumini wa kanisa hilo wakishangilia, alisema, “yaani nikimbie huyu mwanadamu ngulu mbili kama mimi. Anayekwenda chooni kama mimi. Mimi namwogopa huyo ambaye anayefinyanga bingu na nchi.”

“Aliyenifanya na mimi nitembee, amenifanya na mimi niombee, amenifanya na mimi niwe, amenifanya na mimi nivae suti, amenifanya na mimi nichanue. Mimi nikuogope wewe, nitakuua huuuuu, mimi nikifa nakwenda mbinguni, wewe ukifa unakwenda jehanamu,” alisema

Akiendelea kuhuribi, Nabii Mwingira alisema, “halafu ujue uhai wangu uko mikononi mwa bwana, kwa hiyo Mungu ataamua kati yangu na wewe nani afe. Kwa sababu mimi nakwenda binguni, wewe unakwenda jehamanu halafu unataka kuniua mimi?

“…lakini mwamuzi wa mbingu na nchi yupo juu halafu unataka kuniua, halafu wewe umeumbwa kama mimi, Mungu ataamua kati yangu na wewe nani afe,” alisema

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za SiasaTangulizi

Shibuda amlima waraka mzito Bulembo

Spread the loveMKONGWE wa siasa nchini, John Shibuda amemshukia kada maarufu wa...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

error: Content is protected !!