July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Polisi yazuia maandamano ya kumpinga Magufuli

Spread the love

JESHI la Polisi mkoani Mwanza, limepiga maarufuku maandamano ya amani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ya kupinga matokeo yaliyompa ushindi, Rais mteule wa awamu ya tano, John Magufuli. Anaandika Moses Mseti, Mwanza … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo na Kamanda wa Polisi Mkoa wa mwanza, Kamishna Msaidizi, Charles Mkumbo, wakati akizungumza na waandishi wa habari, ambako amesema ni marufuku kwa mtu yeyote yule kuandama kesho.

Amesema licha ya chama hicho kufikisha barua ya kuomba kibali cha kufanya maandamo ya kupinga matokeo ya Magufuli na kwamba Polisi hawatasita kuwachukulia hatua za kisheria wale wote watakao fanya maandamano.

Mkumbo amesema kuwa endapo mtu ama kikundi chochote kile kitabainika kufanya maandamano, watakuwa wamevunja sheria za nchi, hivyo Polisi haitaka kuwa nyuma kuwachukulia hatua za kisheria.

Hata hivyo Mkumbo alidai kwamba Rais mteule, John Magufuli amechaguliwa na wananchi walio wengi na kutangazwa na Tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC), iweje watu wachache wapinge matokeo hayo.

“Wao wanadai eti… mgombea wao ndiye kashinda (Edward Lowassa), kwamba hawakubaliani na matokeo hayo, sasa maandamano yoyote yale ni maarufuku kufanyika hapa Mwanza,” amesema Mkumbo.

Katibu wa Chadema, Wilaya ya Nyamagana, Rehema Mkoha, akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu, alisisitiza kufanyika kwa maandamano hayo leo na wamejipanga kupinga matokeo hayo.

“Sio kila kitu mpaka uruhusiwe na ukipigwa maarufuku ndo uache kufanya maandamano, hapa ninapoongea na wewe tupo kwenye kikao cha kutoa maamzi ya kufanya kesho maandamano,” amesema Rehema.

error: Content is protected !!