JESHI la Polisi Mkoa wa Dodoma limewakamata wagombea ubunge na udiwani kutoka Chama cha Demokraaia na Maendeleo (Chadema) waliokuwa wanakwenda Ofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) zilizopo Njedengwa Dodoma kufuatilia rufaa zao. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma…(endelea).
Polisi wamewakamata leo Jumamosi tarehe 5 Septemba 2020 wakiwa kwenye gari aina ya Haice eneo la Makulu majumba tatu baada ya kuwakuta askari polisi waliokuwa na silaha za moto huku wakiwa na gari lililokuwa na mbwa wa polisi.
Awali, gari hiyo iliyokuwa imewabeba wagombea hao pamoja na baadhi ya waandishi wa habari iliwafuata wabunge hao ofisi za Chadema Kanda ya Kati na kuanza safari ya kwenda ofisi za NEC.
Baadhi ya waliokamatwa na wako Kituo Kikuu cha Polisi Dodoma ni kutoka majimbo ya Kilombero, Kilosa, Nzega Vijijini, Songea, Ukonga, Ludewa, Bahi pamoja na madiwani.
Kwa mujibu wa NEC, zaidi ya rufaa 550 zinakatwa na wagombea udiwani na ubunge ambazo wanazifanyia kazi.
Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online na MwanaHALISI TV kwa habari zaidi
Habari safi na makini.