Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Polisi yatia neno tahadhari ya ugaidi iliyotolewa na Marekani
Habari Mchanganyiko

Polisi yatia neno tahadhari ya ugaidi iliyotolewa na Marekani

Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, David Misime
Spread the love

 

JESHI la Polisi nchini Tanzania limesema hali ya ulinzi na usalama wa nchi ni shwari kwani limeendelea kudhibiti matukio makubwa yanayoweza kuleta hofu kwa wananchi. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa iliyotolewa leo Alhamisi tarehe 26 Januari kwa vyombo vya habari, Na Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, SACP David Misime, imekuja siku moja baada ya Ubalozi wa Marekani kutoa tahathari kwa watu wake juu ya uwezekano wa kutokea uhalifu wa kigaidi maeneo yanayopendwa kutembelewa na watu wengi.

Jeshi la polisi limesema lilianza kufuatilia taarifa hizo na kuwataka wananchi waendelee kuwa watulivu na kuendelea na shughuli zao kama kawaida.

“Jeshi la polisi Tanzania tulianza kuifanyia kazi taarifa hiyo kwa kina toka ilipoanza kusambaa katika vyombo vya habari… itakapobainika jambo lenye kutia shaka au atakapoonekana mtu mqenye kutia shaka kutokana na mienendo yao, basi taarifa hizo ziripotiwe kwa haraka ili kufanyiwa kazi, ” imeeleza taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imeeleza mikakati yake ya kuhakikisha wanabaini na kuzuia ubalifu kwa kiwango kikubwa zaidi kwa mwaka 2023.

Ametaja mikakati hiyo kuwa ni pamoja kutoa elimu kwa umma ili kuongeza uelewa wa wananchi wa namna ya kushirikiana na jeshi la polisi kuzuia uhalifu kabla haujatokea.

“Kupitia ushirikiano wa wananchi utafiti unaonesha tutaweza kuwa na vyanzo vingi zaidi vya kupata taarifa nyingi zaidi za kuzuia,” amesema SACP Misime.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

error: Content is protected !!