February 27, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Zitto Kabwe akamatwa Dar

Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe

Spread the love

KIONGOZI wa chama cha ACT- Wazalendo, Zitto Zubery Kabwe, amekamatwa na jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Taarifa kutoka kwa watu waliokaribu na mwanasiasa huyo machachari nchini zinasema, kwa sasa Zitto amepelekwa Kituo cha Polisi Oysterbay kwa mahojiano zaidi.

Inaelezwa kuwa Ziito amekwenda kuhojiwa juu ya madai yake kuwa raia zaidi 100 wameuwa na Polisi katika Kijiji cha Mpeta, Wilayani Uvinza, Mkoani Kigoma.

Zitto alitoa madai hayo Jumapili iliyopita, katika mkutano wake na waandishi wa habari.

Habari kamili fuatilia: www. MwanaHALISI Online.com, hivi punde.

error: Content is protected !!