July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Polisi yakusanya mamilioni kwa faini Dar

Spread the love

JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limetoa taarifa kuwa litaendelea kupambana na uhalifu wa kutumia silaha, kudhibiti dawa za kulevya na kuwatoza faini madereva wanaoendesha kwa uzembe, anaandika Faki Sosi.

Akizungumza na waandishi wa habari, Simon Siro, Kamishna wa Polisi Kanda Maalimu ya Dar es Salaam, amesema kuwa Jeshi hilo limekamata silaha mbili ikiwemo SMG iliyokatwa mtutu yenye namba 56-1 2803795 ikiwa na risasi 24 na Bastola moja.

Amesema kuwa silaha hizo zimekamatwa baada ya majambazi wawili kukamatwa katika tukio la kupora shilingi 12 Milioni kwa David Isack(32) eneo la uwanja wa ndege.

Isack alikuwa akihamisha fedha hizo kutoka benki ya NMB kuzipeleka Benki ya DTB akiwa njiani majamabazi hayo yakiwa na pikipiki mbili aina ya boxer MC.729, ATZ na MC 557 AZK yalimzingira na kumpora fedha hizo.

Aidha Siro amewaambia waandishi kuwa polisi wamefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wa ujambazi wanne eneo la Buguruni kwa Mnyamani wanaodaiwa kuwa wamekuwa wakijihusisha na shughuli za ujambazi kwa kutumia silaha ,

Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Mohamed Hassan(21), Hamiss Ally(20), Adam Salum(23) na Bakari Hamis(19).

Kwa wakati mwengine jeshi la polisi limekamata Gongo lita 160, Bangi kete 250 puli 110 pamoja na watuhumiwa 130

Kwa upande wa makosa ya usalama barabarani Sirro amesema kikosi hicho kimekusanya takribani moja billion, baada ya kukamata magari 32528, pikpiki 4046, daladala 23264 na magari mengine ni 9,264 kutokana na makosa ya barabarani kuanzia Januari Mosi hadi Februari 22 mwaka huu.

error: Content is protected !!