January 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Polisi yajitamba kuimarisha ulinzi Dar

Kamanda mstaafu na Mwenyekiti wa kamati ya nidhamu klabu ya Simba Suleiman Kova

Spread the love

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limeumarisha ulinzi kipindi chote cha sikukuu ya Idd Elfitry ili wananchi washerekea kwa amani na utulivu. Anaandika Faki Sosi, DSJ … (endelea).

Hayo yameelezwa leo na Kamanda wa Kanda hiyo Seleiman Kova alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuwaondolea wananchi wasiwasi.

Kova amesema jeshi limeweka mikakati mbali mbali ya kukubaliana na uhalifu unaojitokeza kipindi cha sikukuu  ikiwa pamoja na kushikiana na vyombo mbalimbali vya ulinzi na usalama

Amesema kuwa wamepanga kutumia kikosi maalumu cha intellijinsia,Kikosi Kutuliza ghasia (FFU),Askari wa mbwa na farasi na doria za askari wa miguu na pikipiki ili kuzuia matukio au mipango ya kufanya matukio ya uvunjifu wa amani.

Aidha, amesema  ulinzi utaimarishwa sehemu za kufanyia ibada ,kumbi za starehe,fukwe za bahari na kuzitaka familia kutotelekeza makazi yao bila kuacha ulinzi.

Ikiwa ni pamoja  na kuwataka wazazi wasiwache watoto wao wakiogelea  katika fukwe bila uangalizi wao huku akipiga marufu  disco toto kwenye mkusanyiko mkubwa.

“Jeshi halita  vumilia aina yoyote ya uhalifu au majaribio ya matukio ya uvunjifu wa amani na jeshi litapambana na watu ambao wanatumia siku hizi za siku kuu kama siku za kufanya  uhalifu na wale wanywaji wa pombe wasinywe kupitiliza  ni hatari” amesema Kova

Amesema  wananchi watoe taarifa wakihisi uvunjifu wa amani na matukio kupitia namba zifutazo  RPC Ilala  :Lucas  Mkondya  0715009980 ,RPC Temeke  :Andrew Satta  071500979 na RPC  Kinondoni Camilius Wambura  0715009976.

Hata hivyo amesisitiza jeshi linaendelea na msako mkali kufuatia tukio la kuuawa kwa askari wanne na raia watatu lilotokea katika kituo cha Polisi  Sitakishari  na raia watatu wiki hii.

error: Content is protected !!