August 15, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Polisi wazidisha danadana tuhuma za Sosopi.

Spread the love

Jeshi la Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam limeendelea kupiga danadana tuhuma zinazomkabili Patrick Ole Sosopi, Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha), anaandika Josephat Isango.

Taarifa zilizopatikana hadi jioni ya leo zinasema Sosopi ameambiwa aripoti tena kanda maalumu ya Dar es Salaam tarehe 19 Augosti kwa sababu upepezi wa suala lake bado unaendelea.

Hii ni mara ya nne Sosopi kuripoti katika kituo hicho akitokea kwake Isimani mkoa wa Iringa.

Akiongea na MwanaHALISI online baada ya kutoka Polisi, amewalalamikia polisi kuwa wanampotezea muda asifanye kazi za siasa kwani kama walimkamata kwanini wasimfikishe mahakamani ili ionekane kama ana hatia au la.

Madai ya Sosopi ni kuwa aliwaambia Polisi kuwa yeye ametoa maoni kama raia mwingine, na kwamba polisi waache kutumiwa na Chama cha Mapinduzi, na vijana wa Chadema wapo tayari kuwafundisha huko huko mtaani ili waache kutumiwa.

Aidha akifafanua madai kwanini alisema ‘kama mbwai na iwe mbwai’ Sosopi amesema kuwa iwe isiwe, wakubali au wasikubali polisi wanapaswa kufundishwa ili waache kutumiwa na CCM.

“Kila ninapokuja Dar es Salaam, natumia gharama zaidi ya laki 2 hadi 3, kwa masuala ya kusafiri na kulala, polisi wanajisikia vizuri kunisumbua, lakini ifike mahali wajue wao ndio wanaharibu jeshi liache kuheshimiwa” alisema.

Walipaswa wawe wametaja kosa langu niwe huru, sisi tunataka tukaanze nao huko mtaani kabla operesheni ukuta haijafika wawe wameelimika wasitumike  na CCM tena, hii nchi ni yetu wote tujaribu kuheshimiana, aliongeza.

Wanatuzuia sisi, wanatushikilia lakini CCM wanatumia mikutano hiyo hiyo kutukejeli, kututukana na kuingiza wanachama wetu kwenye chama chake huku sisi tukiwa tumezuiliwa.

 

error: Content is protected !!