Monday , 26 February 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Polisi wavuruga mkutano wa Chadema Mwanza
Habari za SiasaTangulizi

Polisi wavuruga mkutano wa Chadema Mwanza

Salumu Mwalimu, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zanzibar
Spread the love

JESHI la Polisi mkoani Mwanza limevamia ukumbi wa Hill Front Hotel uliopo Igoma, katika Manispaa ya Nyamagana, kuvunja kongamano la vijana lililoandaliwa na Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha), Jimbo la Nyamagana, anaandika Mwandishi wetu.

Mgeni rasmi ni Salumu Mwalimu, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zanzibar. Pamoja naye wako Viongozi wa CHADEMA Mkoa wa Mwanza, Mbunge wa Viti Maalum mkoani humo Susanne Maselle Makene, pamoja na makamanda mbalimbali wa chama hicho.

Hadi muda huu viongozi hao wamezuiliwa kuingia ukumbini ambako tayari wanachama, wapenzi na wafuasi wamejaa kuanzia saa 5 asubuhi kwa ajili ya kongamano hilo.

Awali polisi walifika maeneo hayo kabla ya msafara wa viongozi, ambapo juhudi zao za kuzuia kongamano hilo ati kwa sababu waliitoa kuwa linafanyika ‘nje’, zilikwama baada ya vijana wa Chadema waliokuwa wakisubiri msafara wa Naibu Katibu Mkuu ufike, kuwaambia polisi waende pia wakazuie kikao cha ndani cha CCM ambacho kinafanyika eneo la wazi kabisa Viwanja vya Grand Hall, jirani na Ofisi za Makao Makuu ya CCM Mkoa, wakati Kongamano la Bavicha linafanyika katika ukumbi ambao uko fenced.

Baada ya kujibiwa hivyo, polisi wale waliondoka. Lakinu mara tu msafara ulipowasili kwa ajili ya ufunguzi wa kongamano, polisi wakarudi na kuzuia viongozi hao wasiingie ukumbini bali wahamishie shughuli hiyo katika ukumbi wa ndani. Mahali hapo hakuna ukumbi zaidi ya huo mmoja ambao uko fenced.

Kongamano hadi sasa halijaanza ambapo viongozi wako nje na wanachama wamejaa ukumbini akisubiriwa RCO ambaye polisi wamesema ndiye atatoa hatma ya kinachopaswa kuendelea.

Yote hayo yanafanyika kinyume kabisa na sheria za nchi. Hakuna mahali popote pale ambapo Jeshi la Polisi linaruhusiwa kwa mujibu wa sheria kuingilia vikao au shughuli za ndani za kisiasa za vyama vya siasa.

Lakini pia ni mwendelezo wa unyanyasaji mkubwa na ukandamizaji wa haki za kikatiba na kisiasa na haki za binadamu unaoendelea nchini ukifanywa na Jeshi hilo kwa maelekezo ya viongozi wa kisiasa kwenye Serikali ya CCM.

Ndiyo maana polisi wanaweza kuthubutu kuzuia kongamano la Chadema linalofanyika katika ukumbi uliozibwa lakini wakaacha kikao cha ndani cha CCM kinachofanyika eneo la wazi nje kabisa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Hamahama Ngorongoro kutikisa maandamano ya Chadema Arusha

Spread the loveMAELFU ya wanachama na wafuasi wa Chama cha Demokrasia na...

Habari za SiasaTangulizi

Waliofariki ajalini Arusha kuagwa siku ya maandamano Chadema

Spread the loveMIILI ya watu 25 waliofariki dunia katika ajali iliyohusisha lori...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali kuiburuzwa mahakamani ajali iliyoua 25 Arusha

Spread the loveMTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), imeitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Samia atoa pole ajali iliyoua 25, kujeruhi 21 Arusha

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu...

error: Content is protected !!